Skip to content
Tags

Heroini

09/08/2013
Shumuya

Heroini,
Heroini safi isiyokuwa na doa.
Biashara kuu ya pili ya Kolonia Santita baada ya kokeini, iliyomfanya Panthera Tigrisi awe tajiri wa kutupwa
katika miaka ya 80.

Advertisements

From → Picha

14 Comments
 1. Heroini (shumuya) hutokana na mmea wa maua uitwao mbaruti-afyuni – oppium poppy – jamii ya mimea ya mibaruti (poppy) inayopatikana katika sehemu mbalimbali za dunia hususan katika bara la Asia. Mbaruti-afyuni ni mmea mrefu wenye kirungu kidogo kwa juu kama tunda hivi, lenye maua kidogo kwa juu yake. Tunda hilo ambalo hujulikana kama tumba au jicho la ua au poppy pod au bud kwa utaalamu zaidi, linapokomaa hupasuka na kutoa maua mazuri mekundu ambayo baadaye hutumika kama mapambo katika nyumba za watu. Licha ya kutumika kama mapambo katika nyumba za watu na katika sherehe za kimila, mbaruti-afyuni hutumika kwa kutengeneza chakula na madawa ya kulevya hali kadhalika: kwa sababu za kiuchumi na kiutabibu. Kabla tunda halijaiva na kupasuka, wakulima – kwa kutumia nyembe maalumu – hulikata kwa kulichanja na kutoa afyuni au utomvu, au kasumba au latex sap au opium, au ‘machozi ya mbaruti’.

  Ndani ya afyuni kuna asilimia 12 ya morfini (na kemikali zingine za kialkaloidi zinazojulikana kitaalamu kama opiates; kama thebaini [paramorphine] na kodini [3-methylmorphine]) ambayo baadaye hushughulikiwa kikemia na kutengeneza shumuya na madawa mengine kwa ajili ya sayansi na utabibu. Kadhalika, baada ya kutoa afyuni yote, ama kwa mikono au kwa mashine, tunda hupasuliwa na kutoa mbegu nyingi ndogondogo zilizokuwemo ndani. Mbegu hizo, zenye mafuta, huweza kuliwa kama chakula au kukamuliwa na kutoa mafuta kwa ajili ya kupikia na matumizi mengine. Afyuni huzalishwa katika maeneo manne tu ya dunia nzima: Afuganistani, Kusini-Mashariki mwa Asia – ikiwemo Bama na Tailandi, Amerika ya Kusini hasa Kolombia, na Sinaloa nchini Meksiko. Afuganistani ndiyo inayoongoza duniani kwa kuzalisha afyuni, kuliko nchi nyingine yoyote ile, ikiwa imefikia mpaka kiwango cha asilimia 90.

  Kutengeneza shumuya si kazi ngumu hata kidogo. Unachohitaji ni kemikali tu za kawaida, pamoja na maji mengi. Baada ya kuvunwa, afyuni huchemshwa na chokaa au kalisi na kutengeneza mchanganyiko wa morfini inayoweza kuyeyushwa na maji. Kisha mchanganyiko huo wa kimiminiko huchujwa na kuchemshwa tena, lakini sasa na madini ya shabu, ili kupata morfini ya poda iliyokauka. Mamafia hupakia poda hiyo katika vifurushi na kuipeleka katika maabara za mafichoni katika milima ya Afuganistani, ambako morfini hushughulikiwa kitaalamu na kutengeneza INN (diacetylmorphine) na BAN (diamorphine) au morphine diastate; ambazo zote ni shumuya. Kutoka Afuganistani INN na BAN husafirishwa mpaka Irani na Pakistani. Huko husafirishwa kwa njia ya anga, maji na ardhi; mpaka Urusi, Ulaya ya Mashariki, Uturuki, China na Afrika ya Magharibi. Uturuki na Afrika ya Magharibi ni vituo vikuu vya usafirishaji wa madawa yanayokwenda Afrika, Ulaya na mabara yote ya Amerika.

  Mtumiaji wa shumuya huweza kuivuta kwa mdomo (si kwa kuichoma kama sigara au kwa kuichoma ndani ya kiko cha kioo au balbu ya taa, au kwa kuichoma kwa kibiriti cha sigara kwenye karatasi ya aluminiamu na kuvuta mvuke wake), kwa pua (snorting au insufflation), kuimeza, kujidunga kwa sindano katika mishipa ya damu, na kujidunga kwa sindano katika sehemu za siri (suppository kwa lugha ya kitabibu). Kuvuta shumuya kwa kutumia karatasi ya aluminiamu na balbu na kiko cha kioo au kwenye kijiko, huitwa ‘chasing the dragon‘. Kuvuta methamfetamini huitwa ‘chasing the white dragon‘.

  Sindano katika vena inalewesha kwa ufanisi zaidi kuliko njia zingine za utumiaji wa shumuya. Njia ya pili kwa ufanisi ni njia ya sehemu za siri, ikifuatiwa na kuchemua au snorting. Sindano huchukua sekunde chache tu kumlewesha mtu, wakati kuvuta kwa pua huchukua mpaka dakika 15. Mtu anapojidunga shumuya, shumuya husafiri katika mkondo wa damu hapohapo na kupenya kinga ya damu na ubongo kichwani. Inapoingia katika ubongo shumuya hubadilika kikemia na kuwa morfini, na kufurika katika sehemu yote ya mfumo wa ubongo inayoshughulika na starehe, na kumfanya mtumiaji ajisikie raha ya kupindukia. Tabia hiyo ikiendelezwa kwa muda mrefu shumuya hubadili muundo na kazi ya ubongo na kumwingiza mtumiaji katika utegemezi na uraibu usio na kifani wa madawa ya kulevya. Ukishakuwa teja umejitia kifungoni. Usipo’kita’ (usipofix), usipopata dozi ya shumuya, utaugua kitu kinaitwa ‘ugonjwa wa shumuya’ (au ‘dope sickness‘). Utajisikia homa, kutetemeka, kutapika na maumivu ya misuli.

  Ma Nang Nyi, mtoto wa Kamishna-mlezi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia U Nanda, alipojidunga sindano ya shumuya na kuzidisha dozi bila kujua huko Bama, alianza kufifia na kuishiwa na nguvu. Kiasi kikubwa cha shumuya kinapofurika katika ubongo wa mtumiaji mfumo wa kupumua huathirika kwa kiasi kikubwa na mwili husahau kupumua. Mtumiaji anakuwa mahututi. Asipofanyiwa huduma ya kwanza haraka (ya kumrudishia fahamu) shumuya itashinda vita na moyo wake utasimama kupiga. Watumiaji wengi wa shumuya huanza na dawa za kupunguza maumivu kama oxycodone (oxys kwa kifupi) ambazo hupatikana kwa wingi katika maduka ya dawa. Miezi minne hivi daktari anapositisha utoaji wa oxys kwa mgonjwa, mgonjwa anakuwa tegemezi wa dawa hizo na kujenga uraibu. Mgonjwa anaposhindwa kupata dawa hizo kihalali kwa maagizo ya daktari huzipata kwa walanguzi wa mitaani na kuzinunua, lakini kwa bei ya juu. Kidonge kimoja cha oxys huuzwa kwa Tsh. 120,000 mpaka Tsh. 200,000 na mtu huweza kutumia hata vidonge vitano kwa siku. Uraibu wa oxys unapoongezeka na mgonjwa hana tena hela ya kununulia vidonge, mgonjwa uhamia katika kuiba kwa ndugu, jamaa na marafiki kukidhi haja ya oxycodone. Huko Marekani kumekuwa na matukio mengi ya watu kuvamia maduka ya dawa na kuiba oxys kwa unyang’anyi, na hivyo wengi kukamatwa na kushtakiwa na kufungwa jela.

  Tofauti kati ya oxycodone na shumuya ni kwamba shumuya hupatikana kwa urahisi, ina nguvu zaidi, na hugharimu kiasi kidogo tu cha pesa. Shumuya na oxycodone zina madhara sawa katika ubongo na uridhishaji wake hautofautiani. Kadiri utakavyotumia ndivyo utakavyohitaji na ndivyo utakavyoumia.

  • This is very nice!

  • Morfini, thebaini na kodini ni alkaloidi zinazopatikana ndani ya afyuni – kutoka kwenye mmea unaojulikana kitaalamu kama Papaver somniferum. Kwa jumla hujulikana kama opiates. Morfini hutengeneza shumuya, thebaini hutengeneza oxycodone, kodini hutengeneza naproxen ambayo ni dawa ya homa. Shumuya hubadilikia ndani ya ubongo kuwa morfini, wakati kodini hubadilikia ndani ya ini kuwa morfini hali kadhalika.

   Chokaa ni slaked lime, kalisi ni calcium lakini kalisi inayotengeneza shumuya ni calcium hydroxide; madini ya shabu ni ammonium chloride.

   Watu hutumia vibaya opiates kuliko kokeini, eksitasi na methi kwa pamoja. Opiates zingine ni kama hydrocodone (ambayo ni dawa ya maumivu), xanax (ambayo ni dawa ya wasiwasi) na percocet (ambayo ni dawa ya maumivu).

   Madhara ya kutumia shumuya kwa sindano ni makubwa kuliko unavyoweza kufikiria. Watu huweza kuugua UKIMWI, homa ya manjano (B, C na delta fulminate), n.k., kwa sababu ya kupoteza fahamu na kuzimia. ‘Chasing the dragon‘ maana yake ni kuvuta shumuya. ‘Dragon‘ ni shumuya, kwa tamaduni za watu wa Asia.

 2. Kupona addiction ya heroini nivigumu sana ni bora utumie hata kokeini au madawa mengine….

 3. watu wengi wanaokufa kwa dawa za kulevya hufa kwa overdose ya shumuya.

 4. rosemerrymalima permalink

  Maelezo ya shumuya yanajitosheleza.Umetuambia chanzo chake. Matumizi yake mpaka madhala yake.

 5. Phoebe Majigo permalink

  shumuya ni madawa hatari zaidi duniani kulingana na reports za umoja wa mataifa na mashirika mengine yanayoshughlika na masuala ya madawa ya kulevya.

 6. Shumuya wangeliiacha itumike kwenye pharmaceauticals pekee na sio sehemu nyingine yoyote; kwa sababu ya madhara yake.

 7. josephat rugamalila permalink

  Kusingekuwepo na madawa ya kulevya watu wangepungukiwa na nini?

 8. Barnabas Hosea permalink

  Hayo ni maelezo muafaka kabisa!

 9. I such as this weblog greatly, It’s a rattling nice billet to read and get a hold of information .

  • garcinia cambogia I am impressed, I must say. Very seldom do I
   encounter a blog that is both educational and entertaining, and let me tell you, you have hit the nail on the head.
   Your thoughts is outstanding; the issue is something that not a lot of people are talking intelligently
   about. I’m very happy that I stumbled across this
   in my search for something relating to it. garcinia
   cambogia reviews

  • garcinia cambogia reviews Thanks for your concepts. One
   thing I’ve noticed is that banks along with financial institutions
   are aware of the spending patterns of consumers and understand
   that many people max out there their real credit cards around the getaways.
   They smartly take advantage of this particular
   fact and start flooding your inbox in addition to snail-mail box by using hundreds of no interest APR card offers soon after the holiday season finishes.
   Knowing that should you be like 98% in the American general public,
   you’ll rush at the one opportunity to consolidate credit card debt and
   switch balances to 0 interest rate credit cards.
   garcinia cambogia reviews

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: