Skip to content

Mtu

09/12/2013

62. Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote.

Advertisements
6 Comments
 1. Je, si kweli kwamba mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote? Labda ni kweli. Labda si kweli. Lakini hebu jiulize. Watu hudhibitiwa namna gani katika uso wa sayari hii? Kwa woga. Woga wa hiki. Woga wa kile. Woga wa chochote. Kimsingi watu huogopa kuishi, kufanya kile wanachodhamiria hasa kufanya, kuishi maisha wanayotaka hasa kuishi. Kwanini? Kwa sababu hutumia akili nyingi kufikiria mawazo ya watu wengine. Hawako huru. Watu wanaojali shida za watu wengine hawako huru kuyafurahia maisha yao, na kwa maana hiyo hawako huru kufanya chochote.

  Kwanini tunajali sana shida za watu wengine? Je, ni woga kwamba endapo tutafanya kitu ambacho si cha ‘kawaida’ tutapoteza heshima yetu? Lakini kawaida ni nini? Nani huamua kitu gani ni cha kawaida au si cha kawaida? Kuujua ukweli unapaswa kuwa na hekima ya maisha. Watu wengi hukosea kufikiria kwamba wanaweza kweli kuwa na furaha katika maisha.

  Tuko huru kufanya chochote pale tunapopoteza kila kitu katika maisha yetu. Fikiria huna chochote katika maisha. Huna kazi. Huna familia. Huna kitu cha kupoteza. Mpaka ufikie hatua hiyo ndipo utakapopata uhuru kamili wa mawazo – kufanya chochote unachotaka katika maisha yako. Hivyo ndivyo tunavyotakiwa kufanya: kuamka, kufumbua macho, kuujua ukweli.

  Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote.

 2. Kwa mfano, una mke au mume na watoto unaowapenda sana. Marafiki zako wamekuja na wazo la kukurubuni: kwenda benki kubomoa ili maisha ya familia zenu yaboreke. Lakini unashindwa kwenda kwa kuhofia kukamatwa na kupelekwa jela, na hivyo kuacha familia yako ikiteseka eti kwa sababu ya uhalifu wako. Ukishindwa kwenda, familia yako imesababisha usiishi maisha unayoyataka. Lakini kama familia yako ingekuwa bazarai, hungezuiwa na chochote kuwa jambazi, ungeishi maisha unayoyataka.

 3. Lakini nani hatari zaidi kati ya hawa wafuatao: Aliyepoteza kila kitu katika maisha yake, au mwenye kila kitu katika maisha yake? Jadili.

 4. Mtu mwenye kila kitu ktk maisha ni hatari sawa na mtu aliyepoteza kila kitu ktk maisha – wote wana power!

 5. Mwenye kila kitu ni hatari zaid kwa sababu ana power ya kufanya chochote atakacho.

 6. phoebemajigo permalink

  mtu aliyepoteza kila kitu katiaka maisha yake ni sawa na mtu aliyehukumiwa kifo – wote ni hatari

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: