Skip to content

Siri

16/12/2013

63. Siri ni siri ya mafanikio.

Advertisements
3 Comments
  1. Kuna sababu ya msingi inayoleta tofauti kati ya madaraja ya mafanikio miongoni mwa maazimio ya watu. Sababu hiyo ni mazoea ya utunzaji wa siri. Zipo sababu nyingi zinazofanya watu wenye uwezo wa kutunza siri wafanikiwe zaidi kuliko watu wasiokuwa na uwezo wa kutunza siri. Hiki ni kitu ambacho watu wengi hawakijui. Unapotambua sababu ya siri kuwezesha mafanikio ya maazimio ya watu, unaweza kuwa na uwezo au weledi wa kutosha juu ya mafanikio yako. Mafanikio siri yake ni siri.

    Katika zama za kale za sanaa za jumbe zilizojificha (‘mystical arts’), kazi zote za kishetani zilikuwa zikifanyika katika uficho wa hali ya juu. Hii ni kweli kwa sababu ya kupindisha ukweli. Mwanamazingaombwe alikuwa akitumia nguvu za kiulimwengu, kuweza kuhitimisha matokeo ambayo kwa kawaida yalikuwa hayawezekani katika macho ya watu wa kawaida. Mazingaombwe, kimsingi, kilikuwa kitendo cha kurubuni watu na kupingana na uhalisia wa makubaliano ya wengi. Kama tunavyojua, uhalisia hupatikana ndani ya ufahamu. Mwanamazingaombwe alikuwa akipingana na ufahamu wa watazamaji wake ili atumie akili yao isiyotambua. Njia pekee iliyokuwepo ni kufanya kazi kwa siri, katika mazingira ya akili iliyolala ya watazamaji.

    Kutokana na kanuni ya hiari (‘the law of freewill’), unapokuwa unajua kitu ambacho mtu mwingine hajui, kitu hicho kiko wazi kubadilishwa na mawazo yako kuwa kitu kingine. Watu wengine wakiwa pia na ufahamu wa hicho kitu unachokijua, kutakuwepo na vita au uvutano wa hiari kutambua umiliki halisi wa hicho kitu mnachokipigania. Kupigania kitu bila kukiuka kanuni ya hiari dhidi ya watu wengine ni kufanya hivyo katika mazingira ambapo watu wengine hawajui; siri. Siri ndicho kitu kinachofanya wengine waonekane wamelala, hawajui.

  2. newworldvision permalink

    Serikali zina siri ndo maana zinauwezo wa kuendesha nchi,na kwa sababu ya siri nyingiazo zimefanikiwa..

  3. Secrecy is power, knowledge is power.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: