Wanaume
79. Wanaume hupenda nyama kwenye mifupa.
Advertisements
79. Wanaume hupenda nyama kwenye mifupa.
From → Falsafa za Enock Maregesi
Enock Maregesi was born in Tanzania. He is the author of KOLONIA SANTITA, a novel. In 2015 he won the Mabati-Cornell Kiswahili Prize For African Literature for KOLONIA SANTITA. The prize has the express goal of recognizing excellent writing in African languages and encouraging translation from, between and into African languages! He lives in Tanzania.
Morgens hupenda mikono mizuri ya wanawake. Murphy hupenda nyama kwenye mifupa.
Falsafa ya Wanaume inadhihirisha kwamba Murphy hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mtoto wa rais Debbie Patrocinio (ukurasa wa 252 wa ‘Kolonia Santita’), kwani Debbie alikuwa mwembamba kuliko mchumba wake Sophia Kaswiga. Murphy alimpenda Debbie kwa sababu ya kazi. Aidha, alimpenda kwa sababu ya matatizo yake. John Murphy hupendelea zaidi wasichana waliojazia kuliko wasichana wembamba, hususan wale wanaojikondesha kwa makusudi.
Hata mwanamke mwembamba ana nyama kwenye mifupa. Falsafa ya Wanaume inalenga wanawake ambao tayari ni wembamba, lakini wanaojikondesha kwa makusudi. Kujikondesha kwa makusudi (kujikondesha kupita kiasi) hupelekea matatizo ya kiafya yanayojulikana kitaalamu kama ‘anorexia’. Debbie, baada ya kufiwa na mchumba wake Marciano Moreno Herrera huko Tijuana, mpaka anakutana na Murphy, alikuwa hajala kwa siku saba: hivyo Murphy kufikiria alikuwa na matatizo ya kujikondesha.