Skip to content
Tags

Kalamu

24/04/2014
Kalamu ya Bastola ya John Murphy

Bastola ya kalamu ya John Murphy Ambilikile aina ya Stinger; iliyotumiwa na Murphy kumuua kinyama jambazi sugu wa CS-Moscow – Tawi la Kolonia Santita nchini Urusi na nchi zote za Ulaya ya Mashariki; na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kusini kama vile Masedonia, Montenegro, Uturuki na Ugiriki – Vladimir, huko Yugo Zapadnaya mjini Moscow, katika dacha ya Kolonia Santita.

Advertisements

From → Picha

2 Comments
  1. Bastola ya kalamu aina ya Stinger (tamka ‘Sting’a’) ni silaha ‘halali’ kwa matumizi ya kawaida ya binadamu huko nchini Marekani hadi hii leo; halali kwa maana ya ATF – Shirika la Pombe, Tumbaku na Silaha la Marekani – kuichukulia kama silaha ya kawaida. Lakini Stinger ya John Murphy haikuwa (wala haijawahi kuwa) silaha ya kawaida! Ilitengenezwa kwa ajili ya matumizi ya Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS – ‘WODEC Intelligence Services’) na kwa ajili ya matumizi ya Kikosi cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC – ‘Executive Action Corps’). Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi moja ndogo kwa wakati mmoja – iliyokuwa na ukubwa wa inchi 0.22 ya mtutu wa bunduki (‘.22 caliber’) – na kidonge kimoja cha ‘cyanide’ (‘potassium suicide pill’): ili akitekwa akimeze na kufa; kuliko kutoboa siri za EAC, na siri za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya. Aidha, Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kufyatua risasi ikiwa imenyooka (Stinger ya kawaida hufyatua risasi ikiwa imejikunja) na kifyatulio chake kilikuwa kwenye kichwa cha kalamu; na ilikuwa na koki mbili: moja kwa ajili ya risasi, na nyingine kwa ajili ya mrija wa kalamu, tofauti na Stinger ya kawaida ambayo ina koki moja, mbele ya kifyatulio. Stinger ya Murphy ilikuwa na uwezo wa kuandika kama kalamu ya kawaida! Ilikuwa na uwezo wa kutumia kiwambo cha kupunguza sauti, kama Stinger za kawaida.

  2. Hata Sophia(mchumba wa Murphy) aliamini kama hiyo ni kalam ya kawaida baada ya kuitumia,lakin bila kujua ni bunduki…!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: