Skip to content
Tags

Ghuba ya Meksiko

20/02/2015
Kiongozi wa Kolonia Santita (Panthera Tigrisi) alipotorokea

Sehemu kubwa ya Bahari ya Atlantiki iliyoingia ndani ya pwani ya bara la Amerika ya Kaskazini, Ghuba ya Meksiko, katika mabonde (‘basins’) ya nchi za Kuba, Marekani na Meksiko – kiongozi wa Kolonia Santita (Panthera Tigrisi) alipotorokea mwaka 1986, baada ya kuilaani serikali ya Meksiko.

Advertisements

From → Picha

One Comment
  1. Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote. Serikali ya Meksiko ilipokataa kukidhi matakwa ya El Tigre (Panthera Tigrisi) ya kubadili katiba ya nchi – kuondoa kipengele cha mkataba wa kubadilishana watuhumiwa na washtakiwa – ili akikamatwa asipelekwe Marekani ambako atafungwa na kufia gerezani, El Tigre aliilaani Serikali ya Meksiko. Kujibu mapigo, ya laana ya maluuni, Serikali ya Meksiko ikawakabidhi makamanda 7 wa Kolonia Santita kwa mamlaka za Marekani, na kuongeza juhudi za kumsaka El Tigre mpaka nje ya Amerika Kusini na Kaskazini. El Tigre, kuikomoa serikali na kuwalipia kisasi makamanda wote waliouwawa na kufungwa na shirikisho, akamuua Mwanasheria Mkuu wa Serikali (PGR) na maafisa 7 wa Jeshi la Polisi la Nchi (PJF) kulinganisha idadi ya makamanda wake waliopelekwa Marekani – halafu ‘akapotea’, kabisa; baada ya kutangaza vita na Serikali ya Meksiko!

    Tume ya Dunia imekuwa ikimtafuta Chui wa Siberia kwa zaidi ya miaka tisa. Bila mafanikio. Ulinzi wa Panthera Tigrisi ni wa kimataifa. Mbali na kulindwa na wananchi wa Oaxaca (kwa sababu ya kuwajengea shule, hospitali, makanisa, na kadhalika), na polisi wa shirikisho (kwa sababu ya vitisho, mauaji na rushwa); El Tigre analindwa na jeshi binafsi la kujihami (‘autodefensa’) la wanajeshi wastaafu zaidi ya 1300! Mbali hali kadhalika na ‘autodefensa’; kiongozi wa Kolonia Santita ana walinzi binafsi makomandoo (48) akiwemo A. Narochnitskaya Belinsky, mtaalamu wa kutengeneza nyambizi wa Urusi, na Nicolas Kahima Kankiriho (‘Kahima the Warrior’) mwanajeshi wa kulipwa wa Uganda – aliyetoroka na El Tigre katika nyambizi ya Jefe de Jefes SPD (‘the Silent Predator of the Deep’), iliyotengenezwa na Belinsky, katika Ghuba ya Meksiko Septemba 16, 1986.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: