Skip to content

FNP90

26/02/2015
Mata Policias

Bunduki fupi, nene, nyeusi, kutoka Ubelgiji yenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi (FN P90) inayojulikana huko Meksiko kama ‘mata policias’ (au ‘kiboko cha polisi’), iliyotumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume na polisi wa Amerika ya Kaskazini na Kusini; inayotumiwa na Kikosi cha Usalama cha Rais wa Marekani (‘Secret Service’) dhidi ya magaidi wanaotumia mavazi ya kuzuia risasi, wanaotishia usalama wa rais wa Marekani.

Advertisements

From → Picha

2 Comments
  1. Wakati Vijana wa Tume wanajiandaa kwenda Meksiko kuvamia makao makuu ya Kolonia Santita ulimwenguni, Mexico City (Makao Makuu ya Kolonia Santita) na Salina Cruz (Maabara Kuu za Kolonia Santita) ulinzi uliimarishwa! Kila sehemu (viwanja vya ndege, mabarabara, mahoteli, migahawa, sehemu za wazi, majengo ya serikali, majengo ya tume na kadhalika) ililindwa barabara na ‘autodefensa’ (jeshi binafsi) na ‘sicarios’ (wauaji wa kulipwa) wa Kolonia Santita! Licha ya silaha za kawaida; kama visu, mapanga, bastola na bunduki za masafa mafupi za ‘shotgun’, ‘sicarios’ na ‘autodefensa’ walikuwa na bunduki hatari (ndani ya makoti na magari yao ya kihuni) za Kalashnikov za Kirusi (AK-74 na AK-47) – ‘cuerno de chivos’ (au ‘mapembe ya mbuzi’) kama zinavyojulikana huko Meksiko; na bunduki fupi, nene za Kibelgiji (FNP90) – ‘mata policias’ (au ‘kiboko cha polisi’) zenye uwezo wa kutoboa kinga ya risasi. FNP90 ni bunduki ya kisasa yenye mwonekano wa wakati ujao inayotengenezwa na Kiwanda cha Fabrique Nationale d’Herstal (FN Herstal) cha Herstal nchini Ubelgiji, kwa ajili ya kujilindia (au ‘self defence’), bunduki yenye uwezo wa kubeba risasi 50 kwa wakati mmoja katika chemba yake.

  2. phoebemajigo permalink

    Like it!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: