Skip to content
Tags

Logan

09/04/2015
Lt. General Edward Lawrence Logan International Airport

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Logan huko Boston nchini Marekani, Kiongozi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia Kamishna Profesa Randall Buchanan Ortega alipopandia ndege kwenda Copenhagen; alipokuwa akienda kuhudhuria Kikao cha Dharura cha Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.

Advertisements

From → Picha

2 Comments
  1. Kamishna Profesa Randall Buchanan Ortega, Kiongozi wa Kanda ya Amerika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Mshauri wa Madawa wa Gavana wa Massachusetts, aliyekuwa na umri wa miaka sitini na tatu, alikuwa miongoni mwa wazee wa tume waliowahi kukumbana na matatizo makubwa kabisa katika maisha yao ya kiutumishi. Kama kiongozi wa kanda Ortega alikuwa na kazi kubwa ya kufanya. Mauaji ya Meksiko yalitokea ndani ya mipaka ya kanda yake, ingawa hakuwa na hakika kama ndicho alichokuwa akiitiwa na Kamishna Mkuu Rais wa Tume ya Dunia Boidin Versnick.

    Ndege ya Shirika la Ndege la Uingereza (BA) ilipokuwa tayari katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Logan huko Boston Mashariki nchini Marekani, Ortega na abiria wengine walisafiri kutokea hapo mpaka London kupitia anga la Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini; ambapo alibadili ndege na kuondoka tena (na BA nyingine) mpaka Copenhagen, alipohudhuria kikao cha dharura cha Tume ya Dunia.

    Randall Buchanan Ortega ni mtu aliyejitolea maisha yake kupambana na madawa ya kulevya duniani kote; hasa katika bara la Amerika ya Kaskazini, alipowahi kunusurika kuuwawa zaidi ya mara ishirini na nne nchini Marekani, Kanada, na Meksiko.

    Kadiri unavyozidi kupanda juu ndivyo utakavyoanguka vibaya. Kadiri unavyozidi kutumia madawa ya kulevya ndivyo madhara yake yatavyokuwa makubwa. Hivyo acha kukingali bado mapema.

  2. It’s beautiful

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: