Skip to content
Tags

Energy

01/05/2015
Godoro ambalo hulainika kulingana na joto la mwili

Godoro la kifahari la Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego kutoka Kentucky nchini Marekani, Energy Opus, lililotengenezwa kwa maziwa ya mti wa mpira wa para, John Murphy na Debbie Patrocinio walipolala kwa dakika arobaini na tano bila kupumzika; baada ya maongezi yao ya faragha, na chai na udohoudoho, katika Ikulu ya Meksiko ya Los Pinos.

From → Picha

One Comment
  1. John Murphy alishangazwa na chumba cha Mtoto wa Rais wa Meksiko Debbie Patrocinio Abrego alipoingia Los Pinos; baada ya kutoka katika Baa ya Jangwa la Simba (Desierto de Los Leones) ya San Ángel, Mexico City. Chumba kilikuwa na jumla ya vyumba vinne. Kilikuwa na kitanda kikubwa cha hadhi ya kifalme. Kilikuwa na makochi ya kumeremeta. Kilikuwa na kompyuta. Kilikuwa na televisheni. Kilikuwa na zulia nene jipya jeupe. Kilikuwa na mapazia ya dhahabu ya Taffeta. Kilikuwa na kofia ya taa ya dhahabu ya Baccarat, na vitu vingine vingi.

    Katikati ya chumba, juu ya kitanda kipana cha ukubwa wa kifalme kilichokuwa na nguzo nne za dhahabu chini ya mapambo ya Frida Kahlo, kulikuwa na godoro kubwa la Energy (Energie) Opus. Godoro hilo, ambalo hulainika kulingana na joto la mwili, lililotengenezwa kwa kutumia utomvu wa mti wa mpira wa hevea au para au sharinga na Kiwanda cha Tempur World cha Kentucky nchini Marekani, lilikuwa na kontua za kukanda mwili wakati Debbie (au mtu mwingine) amepumzika. Kadhalika, juu ya kitanda kulikuwepo na kadi nyingi za maombolezo, na wanasesere wa aina mbalimbali; akiwemo wa chui, mtu na nyoka – ambaye pindi ulipomminya mkiani alikuwa akitambaa kama nyoka wa kweli. Wanasesere hao, wengi, alipewa na Lisa kama zawadi ya kumliwaza kutokana na kifo cha mpenzi wake Marciano.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: