Skip to content
Tags

Mumbai

15/05/2015
Mumbai

Makao Makuu ya Tawi la Kolonia Santita nchini India na nchi zote za Asia na Australia, CS-Mumbai, yaliyopo Mumbai, Maharashtra, India, linaloongozwa na Sanjay Kanaka Ramachandra (baba wa watoto sita) ‘The Satellite’, lililoko chini ya udhibiti wa Kamishna Meja Jenerali U Nanda wa Asia-Australia.

From → Picha

3 Comments
 1. Sanjay Kanaka Ramachandra, ‘The Satellite’, baada ya kutoka Korea ya Kaskazini na Salina Cruz kwa ajili ya kozi maalumu ya ugaidi na kwa ajili ya Kiapo cha Swastika kwa mpangilio huo, alirudi Mumbai kusimamia shughuli za Kolonia Santita za bara la Asia na Australia – kwa uaminifu wa Sheria ya Kitalifa ya Kolonia Santita. Ramachandra, anayeitwa ‘The Satellite’ kwa sababu ya jina lake la mwisho, alipewa pia jukumu la kuyachunga Makao Makuu ya Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia; na kupeleka taarifa yoyote ya kijasusi (inayohusiana na WODEC-Rangoon) Mexico City kwa ajili ya maamuzi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Kolonia Santita Gortari Manuel. Mojawapo ya operesheni kubwa alizowahi kuzifanya Ramachandra kwa niaba ya Kolonia Santita ni kuingiza nchini India mzigo wa tani 350 za majani ya koka, ijapokuwa tani 37 zilikamatwa na mamlaka za kuzuia madawa ya kulevya za India na za Tume ya Dunia, na kusambaza kilo 560 za kokeini safi (isiyokuwa na doa) katika nchi zote za Asia na Australia ndani ya siku 14.

  Ramachandra maana yake ni mwezi. Mwezi ni setilaiti na mwezi unamulika. Ramachandra anaitwa setilaiti kwa sababu ya umuhimu wake katika bara la Asia. Anamulika India na bara zima la Asia, na Australia, kwa niaba ya Kolonia Santita. Ana miaka 44. Ana mke na watoto 6. Ni jambazi aliyekubuhu wa India.

  Ramachandra alikwenda Korea ya Kaskazini na timu ya watu 70 kutoka Kolonia Santita, akiwemo Kahima Kankiriho wa Uganda na Anatoly Narochnitskaya Belinsky wa Urusi, kujifunza mbinu mbalimbali za ugaidi wa kimadawa (‘narcoterrorism’) na ugaidi wa mstuni (‘jungle warfare’).

  Sheria ya Kitalifa ya Kiapo cha Swastika ya Kolonia Santita ni utiifu kamili, woga, umbali (kwa maana ya kuwa mbali na biashara ya mamafia wengine mpaka kwa makubaliano maalumu) na nidhamu ya kutoshirikiana na mamlaka zote za serikali. Ukishtakiwa kwa kosa la madawa au ujambazi ambalo hukufanya, utatumikia kifungo mpaka mwisho bila kushirikiana na polisi (kwa maana ya kutaja aliyehusika au waliohusika na uhalifu huo) hata kama aliyehusika au waliohusika hana au hawana uhusiano wowote na Kolonia Santita. Adhabu ya kuvunja sheria hiyo ni kifo.

 2. Mwishowe Sanjay Kanaka alikamatwa na Tume ya Dunia!.

 3. jennypatranella permalink

  Wonderful!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: