Skip to content

Cyanide

30/07/2015
Cyanide

Kidonge kigumu mno kutengeneza na kinachoua kwa maumivu makali ndani ya sekunde kumi na tano tu, Potassium Cyanide, ambacho pindi kinapokutana na asidi za tumboni hubadilika na kuwa gesi ya ‘hydrogen cyanide’ na kupenya harakaharaka katika mishipa ya damu – gesi ambayo huzuia oksijeni kuingia katika seli hivyo kufanya damu iwe na oksijeni nyingi zaidi, kiasi ambacho hakitaweza kutumiwa tena na mwili – kilichobebwa na John Murphy katika bastola yake ya Stinger kama sumu ya kumuua; ili akitekwa akimeze na kufa ndani ya muda mfupi kuliko kutoboa siri za EAC, na siri za Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya.

Advertisements

From → Picha

One Comment
  1. Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya ‘hydrogen cyanide’. Gesi ya ‘hydrogen cyanide’ ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha ‘cyanide’ atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.

    Kila sumu ina kiuasumu chake. Viuasumu vya ‘cyanide’ ni ‘amyl nitrite’, ‘sodium nitrite’, ‘cyanokit’, na ‘sodium thiosulfate’. Kazi ya viuasumu hivi ni kuzalisha madini mengi ya chuma mwilini. Madini haya yatapambana na maada za rangi za uhai (‘cytochromes’) kwa ajili ya ‘cyanide’, ili ‘cyanide’ ing’ang’anie kwenye kiuasumu badala ya kung’ang’ania kwenye vimeng’enya vya seli za mwilini. Kiuasumu kinaposhinda mpambano huo; ‘cyanide’ hutolewa nje kwa njia ya mkojo, na mwathirika wa ‘cyanide’ hupona kabisa. ‘Sodium thiosulfate’ ndiyo bora zaidi kuliko ‘amyl nitrite’ au ‘sodium nitrite’, na ndiyo bora zaidi kuliko ‘cyanokit’.

    Potassium Cyanide huzuia oksijeni kuingia katika seli, hivyo kufanya seli zisipate hewa – na kufa baada ya muda mfupi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: