Skip to content

SAR

18/09/2015
Bunduki ya Ushindi

Bunduki ya Ushindi kutoka Singapuri iliyotumiwa na Frederik Mogens kupiga mkono wa Panthera Tigrisi uliokuwa na bastola ya SIG Sauer ambayo Tigrisi alitaka kuitumia kuchukua maisha yake mwenyewe, SAR, iliyosababisha mfalme wa madawa ya kulevya duniani atekwe nyara na kukabidhiwa kwa mamlaka za Marekani – kujibu tuhuma za kujihusisha na ukulima na usafirishaji wa kokeini kutoka katika mashamba ya msituni ya Kolombia, mpaka katika mishipa ya damu ya watoto wa Amerika.

Advertisements

From → Mengineyo

2 Comments
  1. El Tigre hakukubali kushindwa kirahisi. Bunduki yake ilipokwisha risasi alichomoa bastola na kuendelea kujibu mashambulizi lakini wote, yeye na Vijana wa Tume, wakawa wanakosana. Kazi ya Vijana wa Tume ilikuwa kumkamata El Tigre na kumkabidhi kwa vyombo vya sheria. Haikuwa kumuua. Lakini Murphy alidhamiria kumuua kwa sababu ya Radia. Nahodha alishaondoa nyambizi zamani sana katika jitihada za kuokoa maisha yake na ya bosi wake. Lakini hakufika mbali. Risasi moja tu ya bunduki ya Mogens ilimpasua kifua, nahodha akaegemea usukani na kuingia bazarai kwa uzembe wake. Murphy akiendelea kupambana vikali na Kahima Kankiriho, Yehuda na Mogens walizidi kumshambulia El Tigre mpaka akakata tamaa kabisa. El Tigre alinyanyua bastola yake na kujilenga lakini pisto ikakohoa kwa kuishiwa risasi. Vijana wa Tume kuona hivyo wakashtuka. Hawakujua kama bastola yake haikuwa na risasi; walijua alitaka kujiua. Hawakutaka ajiue. Kama ni kumuua wangemuua wakiwa naye katika himaya yao. Yehuda aling’oa nyambizi na kuifuata nyambizi ya El Tigre kwa mwendo mkali; Mogens, kipindi hichohicho, akiwa na SAR, akaulenga kwa kutumia darubini (telescopic sight) mkono wa El Tigre uliokuwa na bastola na kufyatua. El Tigre alianguka, huku akigumia, pisto yake ikaruka mpaka majini na kupotea.

  2. Bunduki hiyo hapo juu inaitwa SAR-8, ni muungano wa SAR na G3. Bunduki kama hiyo ndiyo aliyotumia Mogens kumteka nyara bilionea Panthera Tigrisi, mfalme wa madawa ya kulevya duniani.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: