Skip to content

Bibi

04/11/2015
Bibi aliyenilea na kunisomesha

Bibi Martha Maregesi aliishi maisha mazuri sana hapa duniani. Alibarikiwa na Mungu. Aliishi miaka 84 – siku 30660 badala ya siku 25550 tulizopangiwa na Mungu. Katika uhai wake wote, kwa wale wote aliowalea, hakuna mtoto wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna mjukuu wake hata mmoja aliyefariki kabla yake. Hakuna kitukuu chake hata kimoja kilichofariki kabla yake. Bibi yangu ametimiza mwaka mmoja kamili leo hii, tangu amefariki dunia Novemba 4 mwaka 2014 mjini Musoma. Tunamkumbuka leo akiwa amefariki kama tulivyomkumbuka jana akiwa hai. Nguvu ya sala zetu imfanye Mwenyezi Mungu aendelee kumsamehe dhambi zake zote, na amweke mahali anapostahili, Amina.

Advertisements
One Comment
  1. Tumepata rais mpya wa nchi, yule aliyekuwa waziri wa ujenzi, John Pombe Magufuli. Alikuwa akishindana vikali na aliyekuwa waziri mkuu, Edward Ngoyai Lowassa, ambaye baadaye alihamia chama cha upinzani cha CHADEMA – baada ya jina lake kuenguliwa katika kinyang’anyiro cha kutafuta mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, CCM.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: