Skip to content
Tags

Jua

02/05/2016

171. Dunia huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka jua. Jua huzunguka kwenye mhimili wake na huzunguka falaki. Dunia hutumia takriban siku moja kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban mwaka mmoja kuzunguka jua. Jua hutumia takriban siku ishirini na tano kuzunguka kwenye mhimili wake, na hutumia takriban miaka milioni mia mbili na hamsini kuzunguka falaki. Yoshua alisimamisha jua ili lisizunguke kwenye mhimili wake na lisizunguke falaki. Kwa sababu jua lilisimama, kila kitu kilichoathiriwa na jua hilo kilisimama pia ikiwemo dunia. Hata hivyo, kwa sababu tukio la Yoshua kusimamisha jua na mwezi yalikuwa maajabu kutoka kwa malaika wema, malaika wema ndiyo wanaojua kwa hakika nini kilitokea. Yoshua alikuwa sahihi kusema jua lisimame si dunia isimame. Mungu aliweza kusimamisha jua kwa ajili ya Yoshua kuwashinda maadui zake, kwa sababu aliamini. Mungu anaweza kusimamisha jua kwa ajili yako kuwashinda maadui zako, ukiamini. Mungu anapokuwa na wewe matatizo yako yako matatizoni.

Advertisements
3 Comments
  1. Falaki maana yake ni kundi la nyota na sayari ikiwemo dunia. Falaki yetu inaitwa Njiamaziwa, ‘the Milky Way galaxy’, yenye mabilioni ya mifumo ya jua ukiwemo wa kwetu. Mungu alisimamisha jua katika falaki ya Njiamaziwa kwa ajili ya Yoshua, ili apate muda wa kutosha kuwashinda maadui zake – wanajeshi wa mataifa matano. Kila mtu alishangaa sana kipindi hicho. Kila mtu anashangaa sana kipindi hiki. Mungu akikubariki watu watasema wewe ni mchawi. Hawatajua nini kilitokea. Kwani kwa Mungu hakuna kinachoshindikana. Mungu aliweza kutenda miujiza kwa ajili ya Yoshua, na kwa ajili ya wana wa Israeli huko Gibeoni na huko Aiyaloni, anaweza kutenda miujiza kwa ajili yako popote pale ulipo. Mungu anachotaka kutoka kwako ni imani ya kweli juu yake, kwa mwili na kwa roho yako yote.

  2. Sayari yetu hujulikana kama Dunia na jua letu hujulikana kama Sol. Dunia imo ndani ya mfumo wa jua wa Sol. Mfumo wa jua wa Sol umo ndani ya mfumo wa jua wa Sol Sector au Solar Interstellar Neighborhood, kwenye wenzo wa Orion wa falaki ya Njiamaziwa, wenye mifumo ya jua zaidi ya 40 ikiwemo Alpha Centauri, Nemesis, Procyon na Sirius. Solar Interstellar Neighborhood imo ndani ya falaki ya Njiamaziwa yenye nyenzo nne zinazozunguka kwa pamoja na falaki nzima. Falaki ya Njiamaziwa imo ndani ya kishada (‘cluster’) chenye zaidi ya falaki 55 ikiwemo Andromeda, Leo A, M32 na Triangulum, kinachojulikanacho kama ‘the Local Galactic Group’. ‘The Local Galactic Group’ imo ndani ya mfumo wa kishada kikubwa zaidi kiitwacho Virgo Supercluster, chenye makundi zaidi ya 100 ya falaki. Virgo Supercluster imo ndani ya mfumo mwingine mkubwa zaidi wa vishada uitwao Laniakea (Local Supercluster) wenye vishada zaidi ya 500 vya falaki. Hapo ndipo mwisho wa ulimwengu wetu unaoweza kuonwa na wanasayansi wetu. Kutoka duniani mpaka Laniakea ni umbali wa kilometa bilioni trilioni 250.

  3. Dunia – Mfumo wa Jua wa Sol – Solar Interstellar Neighborhood – Njiamaziwa – Local Galactic Group – Virgo Supecluster – Local Supercluster – Ulimwengu unaoonekana – Ulimwengu. Huu ndiyo ukoo wa dunia yetu. Chochote alichokifanya Yoshua kilitokea katika ukoo huu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: