Skip to content
Tags

Tutalalaje?

22/08/2016

187. Kama Shetani hawezi kulala sisi tutalalaje? Pambana hadi siku ya mwisho.

Vita ya Shetani na Mungu inatuathiri zaidi sisi wanadamu – na hapo baadaye itamuathiri Shetani pia. Vita hii haiwezi kuisha hadi siku ya mwisho, Yesu Kristo atakaporudi kuwachukua wateule wake. Pambana kwa njia ya maombi hadi siku ya mwisho kwa sababu adui tunayepambana naye hana muda wa kupumzika. Pambana kujiombea na kuwaombea wengine waliohai, na hata wale ambao bado hawajazaliwa, kabla mafuta ya dunia hii hayajalipuka. Usiishi kama adui wa msalaba wa Yesu Kristo, badala yake, ishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo. Kuishi kama rafiki wa msalaba wa Yesu Kristo ni kupinga majivuno yote ya Shetani kwa upendo uliotukuka wa kujishusha au kujidharirisha, kutokutetereka hata kidogo na tamaa za ulimwengu huu kwa upendo mkubwa wa umaskini, na kutokuyumba wakati wa matatizo kwa sababu wakati wa amani ulijilimbikizia imani.
Pambana na Shetani kwa upanga wa imani ambao ni ukweli kwani ukweli ndiyo utakaokuweka huru.
Kabla ya uasi, Mungu alimpa Shetani na wasaidizi wake ambao ni mapepo mamlaka makubwa juu ya kila kitu hapa duniani; kuanzia angahewa la dunia hadi ardhi ya dunia nzima nasi wakazi wake tukijumuishwa. Abadani tusisahau kwamba, kwa kiasi kikubwa, kupambana kwetu kama Paulo anavyosema ni dhidi ya hawa mapepo na mfalme wao ambaye ni Shetani. Tunaishi katika eneo ambapo hata wao wanaishi.
Hawa mapepo wabaya huwatumia maadui wa msalaba wa Yesu Kristo kutekeleza mipango yao kwa lengo la kuwaangamiza marafiki wote wa msalaba wa Yesu Kristo, wanashawishiwa kwa kiasi kikubwa na hizo mamlaka za kimapepo, na kwa sababu wamedanganywa, hawajui hata kidogo kama Shetani anawatumia! Inawezekana hawajatwaliwa na mapepo lakini wanashawishiwa na mapepo kutenda kinyume na mapenzi ya Mungu kwa wanadamu wote.
Jambo ambalo Mungu anataka tulitambue ni kwamba hatuko wenyewe katika bahari hii ya hewa. Hata nyangumi na wazira waovu wanapozunguka huko na huko baharini, ambao pia ni mapepo, wanaochukuliwa kama viumbe wabaya na wachafu na wala mizoga, wanaishi katika bahari hii ya hewa pamoja na sisi. Ni muhimu, kwa ajili ya ustawi wetu wa kiroho, kusikia onyo la Paulo katika Waefeso 6:10-12 kwamba vita yetu si dhidi ya hawa viumbe, na wanapambana usiku na mchana kutetea kile ambacho wanaamini ni cha kwao kwa sababu ya haki ya kuwepo hapa kwanza kabla yetu. Dunia, Biblia inatwambia, ilikuwa makazi yao ya kwanza (Yuda 1:6, KJV). Wanatuchukia kwa sababu taratibu tunakuwa Baba na Mwana, na kwa sababu wanajua hii dunia, urithi wetu, itachukuliwa kutoka mikononi mwao na kukabidhiwa kwa wale ambao ni watoto wa Mungu, wale ambao ni marafiki wa msalaba wa Yesu Kristo.
Usipoangalia kwa undani sana, mapepo wanatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kuwaona. Aidha, wanaweza, bila hata sisi kujua, kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi. Watu wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani na mapepo wake hawataki tujue kama wanatudanganya au wameshatudanganya tayari, na hawataki tujue kama wako hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini. Licha ya hili jambo kutokea katika maisha yetu, Shetani bado anaweza kutudanganya hadi pale tutakapoerevuka kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha kwamba udanganyifu huo hautatokea tena.
Hata hivyo, Shetani anaweza kutudanganya kupitia tamaduni zetu tulizozaliwa nazo. Utamaduni, dunia tunapoishi, ndiyo chanzo cha udanganyifu huu. Yesu Kristo alikufa msalabani ili tupate uhuru kutoka kwa Shetani. Chukua hatua sasa kwa sababu Shetani anaweza kukuteka, na kukufanya mtumwa tena.
Damu ya Yesu Kristo ina nguvu katika ulimwengu wowote ule uliowahi kuumbwa na Mwenyezi Mungu. Itumie!
Advertisements
One Comment
  1. Adui wa msalaba ni yule anayeipenda dunia badala ya Mungu, na rafiki wa msalaba ni yule anayempenda Mungu badala ya dunia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: