Skip to content

Mafanikio Ya Kweli Yanatokana na Nani Unaye

25/10/2016

mafanikio-ya-kweli

Kuna mafanikio ya aina mbili hapa duniani: Mafanikio ya Shetani na mafanikio ya Mungu. Mafanikio ya Shetani ni rahisi kupata na ni ya kitumwa. Mafanikio ya Mungu ni magumu kupata lakini ni ya hakika. Mungu akikubariki, pesa inaongezeka kama inavyoongezeka saa.

Ukiwa na mafanikio ya Shetani hayo si mafanikio ya kweli. Ukiwa na mafanikio ya Mungu hayo ndiyo mafanikio ya kweli. Mafanikio ya kweli hayatokani na NINI unacho. Mafanikio ya kweli yanatokana na NANI unaye. Yesu Kristo alikuwa maskini, hakuwa na kitu; lakini alikuwa tajiri, alikuwa na Mungu ndani ya moyo wake.

Yusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi.

Advertisements
One Comment
  1. Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: