Skip to content
Tags

Mwaka Mpya

02/11/2016

mwaka-mpya

Kitu cha kwanza kufanyika mwanadamu anapozaliwa ni kuvuta pumzi ya kwanza katika mapafu ya mwili wake. Cha mwisho kufanyika kabla ya kufa ni kutoa pumzi ya mwisho katika mapafu ya mwili wake. Pumzi iliyoingia kwanza baada ya kuzaliwa, itakuwa ya mwisho kutoka kabla ya kufa. Pumzi ni bora kuliko muda halafu pumzi ni uhai. Bila uhai watu hawataweza kusherehekea mwaka mpya au kufanya chochote. Likumbuke jina la Mwenyezi Mungu katika kila pumzi unayoingiza na kutoa.

Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo.

 

2 Comments
  1. Biblia inatuambia kuwa tuombe bila kukoma (1 Wathesalonike 5:17). Lakini tutaombaje bila kukoma? Njia mojawapo ya kufanya hivyo ni kutumia ‘maombi ya pumzi’ kila siku kama ambavyo Wakristo wengi wamekuwa wakifanya kwa karne nyingi. Unachagua sentensi fupi au maneno rahisi kuhusu Yesu unayoweza kuyasema na kuyarudia kimoyomoyo kila siku katika kila pumzi inayoingia na kutoka ndani ya mapafu yako. Kwa mfano: “Asante Yesu.” “U pamoja nami.” “Nataka kukujua.” “Napokea neema yako.” “Nakutegemea wewe.” “Mimi ni wako.” “Nisaidie nikuamini.” “U Mungu wangu.” “Naishi kwa ajili yako.” “Nisamehe dhambi zangu zote.” Fundisha akili yako kumkumbuka Mungu kila wakati.

  2. ‘Kusherehekea’ maana yake ni kumsifu na kumshukuru Mungu kila wakati, pumzi inapoingia na kutoka ndani ya mapafu yako.

Leave a reply to Enock Maregesi Cancel reply