Skip to content

Haki na Hekima ya Mwenyezi Mungu

05/12/2016
202. Matatizo ya kijamii, kimiiko, kimaadili, kisiasa, na kiroho; hayataweza kutatuliwa kwa pesa, vikao vya kifamilia, haki za binadamu, usalama wa taifa, au nguvu za kijeshi. Yataweza kutatuliwa kwa haki na hekima ya Mwenyezi Mungu.
 
Israeli ilifikia kikomo cha kipindi chake kikubwa cha mafanikio tangu enzi za Sulemani. Taifa lilikuwa tajiri. Lilikuwa na nguvu. Lilikuwa na silaha nyingi na nzuri zaidi. Lilikuwa taifa lililojidai kwa uwezo wake mkubwa wa nguvu za kijeshi, hekima, ujasiri, utajiri, na faida za kimkakati. Nani angeweza kushindana na Israeli? Lakini Mungu hunguruma onyo kwamba uwezo wote mkubwa wa asili wa taifa, ujuzi waliojipatia, na sifa bora zaidi havikuweza kulisaidia taifa la Israeli. Watu huona nguvu ya taifa katika utajiri wake, idadi yake ya watu, silaha za kijeshi, teknolojia, na maarifa. Lakini Mungu huangalia haki.
 
Kwa vile taifa la Israeli lilipoteza haki yake ya upendeleo, Mungu aliahidi kuliharibu kama alivyoyaharibu mataifa ya Waamori na Wamisri. Watu wa Israeli walishafika mbali sana kiasi cha Mungu kutokutegemea tena toba kutoka kwao. Kuna muda wa fursa na kuna muda ambao fursa haipo tena. Nafasi ya Israeli ya kutubu ilishafikia mwisho.
 
Kama alivyokuwa amepigana vita vyao kwa ajili yao katika siku za nyuma sasa Mungu alipigana nao. Pamoja na ujasiri na utaalamu wao wote wasingependelewa tena. Mambo ambayo mwanzo yaliipa Israeli nguvu katika vita yaliwageukia.
 
Israeli, kama adhabu kwa uozo wake wa kiroho na kimaadili, ilivamiwa na Ashuru katika mwaka wa 721 BC na kuangushwa vibaya katika vita hiyo kubwa. Waisraeli waliosalia walitekwa na kupelekwa uhamishoni ambako inaonekana walitoweka kabisa katika uso wa dunia hii. Hili lilikuwa ni jibu la Mungu kwa dhambi na uasi wao.
 
Sababu ya kupanda na kuanguka kwa mataifa ni ya kimaadili na kiroho. Hakuna taifa linaloweza kutegemea nguvu na mali zake ili kujiokoa kutokana na madhara ya ukiukwaji wa maadili.
 
Dhambi ikizidi katika taifa, Mungu ataliangamiza. Taifa likitenda haki, Mungu ataliinua.
Advertisements
One Comment
  1. Uovu ni aibu kwa taifa zima!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: