Skip to content

Matumizi Sahihi ya Alama ya Nukta Katika Maneno Yaliyofupishwa

07/12/2016

nukta

Nukta hutumika kuwakilisha herufi zilizofichwa katika ufupisho au uminywaji wa neno au maneno husika. Hakuna haja ya kuweka nukta katika neno lililominywa, lakini kuna haja ya kuweka nukta katika neno lililokatwa.

Kwa mfano, neno ‘Mister’ kifupi chake ni ‘Mr’ – bila nukta mbele ya ‘r’ – kwa sababu ‘M’ na ‘r’ zimeminywa hivyo kuficha herufi ‘i’, ‘s’, ‘t’, na ‘e’ na kutengeneza ‘Mr’! Ukiweka nukta mbele ya ‘Mr’, hiyo nukta haitakuwa na maana – kwa sababu haitawakilisha chochote.

Lakini neno ‘Mheshimiwa’ kifupi chake ni ‘Mhe.’ – pamoja na nukta mbele ya ‘e’ – kwa sababu ‘Mheshimiwa’ imekatwa hivyo kuficha herufi ‘s’, ‘h’, ‘i’, ‘m’, ‘i’, ‘w’, na ‘a’ na kutengeneza ‘Mhe.”! Ukiweka nukta mbele ya ‘Mhe.’, hiyo nukta itakuwa na maana – kwa sababu itawakilisha herufi zilizofichwa.

Hivyo, weka nukta katika vifupisho vya maneno yafuatayo: Mheshimiwa (Mhe.), Bwana (Bw.), fizikia (fiz.), aghalabu (agh.), kama vile (k.v.), kwa mfano (k.m.), tazama (taz.), Sanduku La Posta (S.L.P.), Mbunge (Mb.), ‘paragraph’ (para.), ‘Drive’ (Dr.) na kadhalika; kwa sababu ni maneno yaliyokatwa. Na usiweke nukta katika maneno yafuatayo: ‘Mister’ (Mr), ‘Doctor’ (Dr), Bibi (Bi), ‘Miss’ (Ms), ‘paragraphs’ (paras), ‘Saint’ (St) na kadhalika; kwa sababu ni maneno yaliyominywa.

Kiingereza cha Marekani hakiifuati kanuni ya nukta katika ufupisho wa neno au maneno. Lakini Kiingereza cha Uingereza kinaifuata. Hata hivyo, watu wengi hufanya makosa ya nukta kwenye vifupisho vya neno au maneno kwa makusudi na wengine kwa kutokujua. Lakini sasa unajua matumizi sahihi ya alama ya nukta kwenye vifupisho vya maneno. Ni juu yako sasa kufuata kanuni ya Kiingereza cha Uingereza au kanuni ya Kiingereza cha Marekani.

Advertisements
Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: