Skip to content

Vipofu wa Kiroho

19/12/2016
204. Watu wengi tu vipofu wa kiroho! Ili tupone lazima tumtii na kumwamini Yesu Kristo, kama Yesu alivyomponya yule kipofu wa Siloamu kwa sababu alimtii na kumwamini, hata kama hatuwezi kuuona uso wake.

Amri ya Yesu ilikuwa rahisi. Na ilikuwa ya kibinafsi, kwa madhumuni ya kipofu peke yake. Aidha, ilihusisha jaribio la utii ambao Yesu alisubiri kuona yule kipofu angejibu nini. Lakini licha ya yeye kutokuwa na uwezo wa kuona huruma katika macho ya Yesu, yule kipofu alitiwa moyo na amri hiyo. Kipofu, kwa namna fulani, alijua kuwa yule aliyesikia sauti yake angeweza kumsaidia.

Amri ya Kristo ilipima imani ya yule kipofu, ikiithibitisha na kuiimarisha. Bila kuchelewa au kusita, kipofu alitii amri ya Mungu: Alikwenda kuosha macho yake katika bwawa la Siloamu na aliona. Wengi wanaweza kuona ni kazi ya kipuuzi kwa mtu ambaye ni kipofu kufanya kazi ndogo kama hiyo ili aone. Lakini kwa vile alitii, kipofu alipona. Baraka huja kupitia utii. Kwa maana nyingine, kipofu alimtii Yesu bila kuona. Lakini matokeo yake, alipata kuona papohapo; ambapo baadaye, hatimaye, alipokea uponyaji halisi wa kiroho.

Injili tunayohubiriwa haina ugumu wowote. Mungu anatutaka tuamini na tunapoamini, tunapopata ufahamu na kuamini kuwa Mwana wa Mungu alikuwa binadamu kama sisi ili sisi tupate kuokolewa, upofu wetu wa kiroho unaanza kuondolewa.

Advertisements
One Comment
  1. Mwamini Yesu ili upate macho ya rohoni!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: