Skip to content

Mpelelezi wa Tume ya Dunia Daniel Yehuda

27/12/2016

yerusalemu

Mpelelezi wa Tume ya Dunia kutoka Yerusalemu, Israeli, Kanali Daniel ‘Yehuda Ben-Asher’ Ebenezer, Daniel Yehuda, alikuwa komandoo wa kitengo cha mauti na utekaji nyara cha Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli (Kidon) kabla ya kujiunga na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC) huko Oslo, kwa makubaliano maalumu kati ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) na Shirika la Kijasusi la Mossad la Israeli.
 
Daniel Yehuda, Mhebrania aliyeishi Givat Ram, Yerusalemu, na mke wake mrembo Hadara na mtoto wao mzuri Navah Ebenezer, alikuwa Ukanda wa Gaza siku alipopigiwa simu na Kiongozi wa Kanda ya Asia-Australia ya Tume ya Dunia U Nanda – kutoka Copenhagen kuhusiana na wito wa haraka wa kuonana na Rais wa Tume ya Dunia. Yehuda aliondoka usiku kwenda Yangon, Myama, ambapo alionana na U Nanda na kupewa maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata. Mbali na maelekezo yote ya kikazi aliyotakiwa kuyafuata, Yehuda alikabidhiwa na Nanda kachero wa Kolonia Santita Mandi Dickson Santana (bila kujua kama Mandi ni kachero wa Kolonia Santita) ili amsindikize mpaka stendi ya mabasi ya Maubin, nje ya Yangon. Baada ya hapo Yehuda alisafiri mpaka Copenhagen ambapo yeye na wenzake walikabidhiwa Operation Devil Cross, ya kung’oa mizizi ya Kolonia Santita duniani kote.
 
Yehuda alifanya kosa kubwa kuonana na kachero wa Kolonia Santita Mandi Santana! Kwa sababu hiyo, picha na sauti yake vilichukuliwa, watu wengi walikufa katika miji ya Copenhagen na Mexico City.
Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: