Skip to content

Kikamilikacho si Kiimarishwacho

31/12/2016

kikamilikacho

Kikamilikacho si kiimarishwacho. Rais wa Tume ya Dunia alilazimishwa, kufanya kazi aliyokuwa amejitolea maisha yake yote kuipigania kwa nguvu zake zote, na utendaji wake mzuri wa kazi uliharibika.

Kitu kikishakamilika hakiwezi tena kuimarishwa ukilazimisha utakiharibu. Rais wa Tume ya Dunia, Boidin Tony Versnick, alitishwa na Umoja wa Mataifa kuondolewa katika wadhifa wake iwapo angeshindwa kumkamata Panthera Tigrisi ndani ya siku saba bila kujali uaminifu, uthabiti, uvumilivu, uadilifu na uchapakazi wake hodari katika Tume ya Dunia. Mbali na ukamilifu huo katika kazi hata hivyo, kilichokamilika kililazimika kuimarishwa. Versnick ndani ya hizo siku saba alipigana kufa na kupona kutetea wadhifa wake, thamani yake ya utu na kujitengenezea nafasi nzuri katika historia ya Tume ya Dunia na ya Umoja wa Mataifa na ya dunia kwa jumla. Hakuzijali tena sifa zake za kazi, hakujali sheria, hakujali vitisho vya Umoja wa Mataifa. Lakini pamoja na kazi nzuri aliyofanya, Boidin Versnick alilazimika kujiuzuru wadhifa wake; nafasi yake ikachukuliwa na Makamu wa Rais wa Tume ya Dunia, Jørgen Vestergaard Laursen, aliyekuwa na umri wa miaka sitini na mchapakazi hodari kutoka Denmaki. Versnick alipigana na Kolonia Santita kwa pupa, licha ya shinikizo la Umoja wa Mataifa. Usimlazimishe mtu kufanya kazi ambayo tayari anaifanya vizuri.

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: