Skip to content

Jangwa la Simba

08/01/2017

los-leones

Desierto de Los Leones au Jangwa la Simba kwa Kiswahili, mgahawa wa watu wakubwa wa Latino, kusini-magharibi mwa Mexico City, katika Kitongoji cha San Ángel, katika Wilaya ya Álvaro Obregón, John Murphy na Frederik Mogens walipokutana na watoto wa wakubwa wa Meksiko Debbie Patrocinio na Lisa Graciano, katika mazingira ya usalama wa hali ya juu wa WODEC Intelligence Services WIS na PSD ambacho ni kikosi maalumu cha ulinzi wa rais wa Meksiko.

Sifa kubwa ya Murphy ni udadisi, lakini kubwa zaidi ni unyamaume. Haogopi kitu. Anaheshimu sheria. Jumatano saa nne asubuhi, Murphy na Mogens walikutana na Debbie Patrocinio Abrego (na rafiki yake mpenzi Lisa Madrazo Graciano) katika Baa ya Desierto de Los Leones, San Ángel, kusini-magharibi mwa Mexico City. Miadi kama hiyo John Murphy huwa haichukulii mzaha hata kidogo! Ndani na nje ya baa: Radia, Yehuda na maafisa wengi wa WODEC-Intelligence walitapakaa kila mahali; kumlinda Murphy na Sajini Mogens. Murphy na Morgens walifurahi kumwona Debbie (kwa mara nyingine) na walikuwa na hamu ya kumjua vizuri yeye na rafiki yake. Muda ulizidi kwenda. Kengele ya hatari ndani ya kichwa cha Murphy ilizidi kulia. Mogens alianza kubadilika! Naam. Kutetea afya na amani ya dunia, Operation Devil Cross ilianza kazi rasmi! Kilichotokea baada ya hapo kilibadilisha historia ya Tume ya Dunia milele.

Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: