Skip to content

Nguzo ya Maisha Yangu ni Historia ya Maisha Yangu

16/01/2017

sina-jinsi

208. Sina jinsi. Nguzo ya maisha yangu ni historia ya maisha yangu. Historia ya maisha yangu ni urithi wa watu waliojifunza kusema hapana kwa ndiyo nyingi – waliojitolea vitu vingi katika maisha yao kunifikisha hapa nilipo leo – walionifundisha falsafa ya kushindwa si hiari. Siri ya mafanikio yangu ni kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu wote. Hiyo wote katika herufi kubwa.
 
Wote katika herufi kubwa (WOTE) si neno la kawaida falau katika nukuu hii ya mafanikio. Linamaanisha kujitahidi kwa kadiri ya uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Watu wengi hujitahidi kwa kadiri ya uwezo wao. Usijitahidi kwa kadiri ya uwezo wako. Jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.
 
Kwa mfano, uko kwenye mashindano ya mbio za mita 100. Utakapofika kwenye kamba, mwisho wa hizo mita 100, utakuwa umechoka sana. Lakini kocha anakuhimiza uendelee mbele mita zingine 50! Unaweza kufika ukiwa mzima au unaweza kufika ukiwa umezimia. Lakini usijali. Ukiendelea mita zingine 50 utakuwa umetumia uwezo wako wote uliopewa na Mwenyezi Mungu. Ukitumia kanuni hiyo katika maisha yako ya kawaida utaweza kufanikiwa.
 
Kila binadamu ana nguvu ya ziada katika mwili wake ijulikanayo kitaalamu kama ATP. ATP (‘Adenosine Triphosphate’) ni molekuli ndogo zaidi iliyoko ndani ya seli ambayo kazi yake ni kutengeneza nguvu ya ziada kwa ajili ya seli, na kwa ajili ya mwili mzima kwa jumla, pale mwili unapoonekana kukata tamaa au kuishiwa na nguvu kabisa. Ni kama jenereta ya umeme kwa ajili ya seli, inayofanya kazi pale umeme wa kawaida unapokatika.
 
ATP hutumika katika kipindi ambapo mtu anakuwa amekata tamaa kabisa katika jambo lolote analolifanya, na yoyote anayetumia ATP ana uwezo mkubwa wa kufanikiwa katika maisha yake. Hivyo, usikate tamaa, jitahidi kwa kadiri ya uwezo wako WOTE.
 
ATP inaweza kukusaidia kupata akili na nguvu ya kufanya jambo ambalo katika hali ya kawaida lisingewezekana. Wakati mwingine unaweza kufanya jambo hata wewe mwenyewe ukashangaa umelifanyaje. Unaweza kwa mfano kufukuzwa na mnyama mkali ukapenya sehemu ambapo, katika hali ya kawaida usingepenya. Sasa usishangae tena. Kilichofanya upenye ni ATP.
 
Kuamsha ATP lazima kwanza ukate tamaa. Lazima kwanza uishiwe na nguvu. Kisha ujilazimishe, au ulazimishwe na mazingira, kufanya jambo.
Advertisements
Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: