Skip to content

Chuki ni Roho ya Mauti

21/01/2017

duma

Chuki ni roho ya mauti. Ifuatayo ni kauli ya Yesu juu ya roho ya mauti: Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi utoe sadaka yako. Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amini nakwambia, hutoki humo kamwe hata uishi kulipa senti ya mwisho.

Usithubutu kutoa sadaka yoyote kwa Mungu ukiwa na kinyongo juu ya mtu. Maneno ya Yesu yanatueleza wazi kuwa Mungu hatazikubali ibada zetu ikiwa tutawachukia wengine. Tunaweza kweli kusema tunamwabudu Mungu katika roho na kweli huku tukiwachukia ndugu zetu? Inawezekanaje moyo ulioelemewa na mzigo mzito kwa kinyongo kumridhisha mtu kama Mungu anavyotaka? Ndani ya mahakama ya Mungu hakuna kesi zilizoshindikana wala si kwamba Mungu amekosa uwezo wa kuona tabia zetu za ndani kabisa. Kila kinachoendelea katika maisha yetu Mungu anakiona. Hivyo, mpende ndugu yako.

Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji; nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. (1 Yohana 3:15).

Advertisements
One Comment
  1. Kauli ya Yesu juu ya roho ya mauti: (Mathayo 5:23-26).

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: