Skip to content

Kuwa Mkristo wa Yesu Kristo

22/01/2017

mkristo

Unapokuwa mbali na Mungu unakuwa mbali na mwanga, unakuwa gizani, unakuwa mbali na joto, unakuwa katika baridi ya milele. Unapokuwa katika baridi ya milele rangi ya ngozi yako itabadilika na kuwa bluu. Macho yako yatakuwa makubwa kama ya nguva. Bluu maana yake ni kuwa mbali na maarifa ya Mungu. Nguva maana yake ni kuwa mbali na utukufu wa Mungu. Kuwa karibu na maarifa ya Mungu na utukufu wa Mungu, usiwe mkristo wa kanisa, usiwe mkristo wa dini, kuwa Mkristo wa Yesu Kristo.
 
Shetani alikuwa kiumbe mzuri kuliko wote mbinguni na ulimwenguni. Mungu alimpendelea. Alikuwa mzuri kuliko malaika wote na alikuwa na nguvu kuliko kiumbe mwingine yoyote yule aliyeumbwa na Mungu, akiwemo binadamu. Lakini alipotupwa kutoka mbinguni kuja duniani, kama Adamu na Hawa walivyotupwa kutoka bustanini kuja duniani, Shetani alipoteza sifa yake. Alipoteza sifa yake kwa sababu ya dhambi aliyoitenda, dhambi ya kiburi, na kwa sababu ya kuwa mbali na utukufu wa mbinguni. Badala ya kuwa kiumbe mzuri kuliko wote, Shetani akawa kiumbe mbaya kuliko wote. Mungu akaahidi kutokumsamehe, kwa sababu yeye ndiye kiumbe wa kwanza kutenda dhambi mbinguni na ulimwenguni, kwani hakushawishiwa na mtu kumuasi Mungu.
 
Kwa vile hatasamehewa, Shetani hatawasamehe wanadamu. Atahakikisha anauwa kila mtu duniani na kumpeleka kuzimu; ambako anaishi yeye, majini, malaika waovu, wana wa Mungu waliotumwa na Mungu kuja duniani kufundisha watu utukufu lakini wakaasi na Mungu akawalaani (au Wanefili) pamoja na nguva. Nguva ni uzao wa Wanefili na samaki wa baharini na malaika wauvu na wanapatikana zaidi katika Bahari ya Atlantiki, katika mwungano wa Bahari ya Atlantiki na Bahari ya Hindi, chini ya Bermuda Triangle, ambako ndiko liliko kanisa kuu la Ibilisi, ambako mkuu wake ni Malkia wa Pwani; na katika Bahari ya Hindi, katika mji wa kuzimu uitwao Hazaramauti, mlima wa majini kwa tafsiri ya Kiswahili au Hadhramaut kwa Kiarabu au Hasarmawethi kwa Kibiblia, chini ya bahari katikati ya Jibuti na Yaman katika Peninsula ya Arabia, ambako mkuu wake ni Malkia wa Bahari ya Hindi. Chini ya Bahari ya Hindi ndipo yalipo makao makuu ya ufalme wa giza hapa duniani.
 
Shetani anatisha. Ana macho makubwa manane: macho ya serafi, macho ya mwanadamu, macho ya simba na macho ya tai, na ana mabawa makubwa sita yenye urefu wa futi sita mpaka nane kila moja. Ana rangi ya bluu, bluu iliyoiva, ambayo ni sehemu kubwa ya rangi ya kuzimu, na macho makubwa kama nguva wa Afrika.
 
Nguva wa Afrika anaitwa Mami Wata au Mama wa Maji. Anapatikana zaidi katika nchi za Afrika ya Magharibi, Kati na Kusini, na Amerika ya Kusini na Kaskazini katika maeneo ya Waafrika. Mara nyingi ni mwanamke lakini kuna sehemu ameonekana akiwa mwanamume.
 
Mtu wa namna hiyo akikwambia njoo nikupige kojoa kwanza ndiyo uende. Maana hujui amekula nini mpaka awe mbaya kiasi hicho. Kukaa karibu na mtu wa namna hiyo ni kujitafutia matatizo makubwa. Kuepukana naye, usiwe mkristo wa Shetani, usiwe mkristo wa kanisa, usiwe mkristo wa dini, kuwa Mkristo wa Yesu Kristo. Kwa maneno mengine, usiwe nasara wa kufuata bendera, usiwe nasara wa kinafiki, kuwa Nasara wa Kweli. Nasara maana yake ni Mkristo.
 
Shetani anaogopa viumbe saba tu hapa duniani na huko mbinguni ukimwondoa Mungu, ambaye anaogopwa na kila kiumbe: Malaika Mikaeli, Malaika Gabrieli, Malaika Rafaeli, Malaika Urieli, Malaika Selafieli, Malaika Ragueli, na Malaika Barakieli, ambao ni malaika wakuu; na tukio ambalo Shetani analiogopa zaidi ni tukio la kurudi kwa Yesu kwa mara ya pili ambalo limekaribia sana, na atafanya kila atakachoweza kabla ya tukio hilo kuchukua roho zetu.
 
Lengo la Shetani ni kuua kila mtu duniani kumkomoa Mungu na malaika wakuu na kutupeleka kuzimu. Lakini atashindwa kwa Jina la Yesu.
Advertisements
Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: