Skip to content

JUA HISTORIA KWA UFUPI YA KOMANDOO NICOLAS KAHIMA KANKIRIHO, ‘KAHIMA THE WARRIOR’, MLINZI BINAFSI WA KIONGOZI WA KOLONIA SANTITA PANTHERA TIGRISI

24/01/2017

nicolas-kahima-kankiriho

Bushenyi, Ankole, Uganda, ndipo alipozaliwa Komandoo Nicolas Kahima Kankiriho; mlinzi binafsi wa Carlos Pulecio Alcántara, kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita; na Panthera Tigrisi, Kiongozi Mkuu wa Kolonia Santita.

Komandoo Nicolas Kahima Kankiriho (‘Kahima the Warrior’) alizaliwa katika Wilaya ya Bushenyi, Ankole, kusini-magharibi mwa Uganda, Julai 24, 1954, mtoto wa tano kuzaliwa, katika familia ya watoto sita ya Nicodemas Kankiriho; mzee wa heshima wa Wabaima, aliyekuwa akisifika sana kwa uchungaji (wa mifugo) na msisitizo mkali wa Ukristo kwa watoto wake wote; hasa Kahima na Yebare, binti yake wa pekee, aliyekuwa wa mwisho kuzaliwa.

Kahima (aliyekuwa na urefu wa futi 6 inchi 3 na aliyekuwa akiongea Kinyankole, Kiswahili, Kiingereza na Kihispania kwa ufasaha), baada ya kutoka Uganda – alipopata mafunzo ya mwanzo ya ukomandoo ya Kiisraeli – alikwenda Urusi na Korea ya Kaskazini ambako, badala ya kufundishwa mbinu za kijeshi za KGB, alifundishwa mbinu kijeshi za CIA; na ambako aliongeza ujuzi wake hadi kiwango cha juu kabisa, kabla ya kwenda Amerika ya Kusini, kama askari wa msituni wa vyama vya kisiasa visivyo rasmi vya magorila wa Kolombia.

Akiwa Kolombia, Kahima alikutana na Eduardo Chapa de Christopher (kiongozi wa zamani wa Kateli ya Diablos de Amazonas, Mashetani wa Amazoni, iliyokuwa ikivilinda vyama vya kisiasa vya magorila vya Americas) ambaye alimwajiri kama mlinzi binafsi na baadaye kama mlinzi binafsi wa Carlos Pulecio Alcántara – kiongozi wa kwanza wa Kateli ya Kolonia Santita. Alcántara alipouwawa, Kahima alihamia kwa Panthera Tigrisi – Kiongozi Mkuu wa Kolonia Santita.

Panthera Tigrisi alikuwa na ulinzi binafsi wa makomandoo 48, na askari mamluki wa Jeshi la Meksiko na Kolombia 1300! Kahima alikuwa bora kuliko wote!

Nicolas Kahima Kankiriho ni jambazi mkubwa kuwahi kuishi katika jimbo la Ankole nchini Uganda.

Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: