Skip to content
Tags

Jithamini

25/01/2017

jithamini

Msamaha si jambo rahisi. Tunapoumizwa, au watu wetu wa karibu wanapoumizwa, tendo la kusamehe linaweza kuwa gumu kuliko matendo yote. Lakini, tambua kwamba msamaha ni mchakato wa muda mrefu unaohitaji ujasiri mkubwa kuuanza hadi kuukamilisha, ongea na watu wanaoelewa maana ya msamaha ili wakuongoze katika mchakato huo. Vilevile, tambua kwamba hata wewe umewahi kufanya makosa na unahitaji msamaha, tambua kwamba suluhisho kamili linahitaji matendo kutoka kwa aliyekosea na kwa aliyekosewa. Wengine hupendwa kwa sababu wanastahili, lakini wengine wanastahili kwa sababu hupendwa. Mungu anatupenda kwa jinsi tulivyo hata kama tunajiona hatustahili. Hivyo, jithamini.

Msamaha ni uamuzi wa makusudi wa kuachilia hisia za chuki au kisasi juu ya mtu au kikundi cha watu ambaye amekuumiza au ambacho kimekuumiza, bila kujali kama anastahili au kinastahili msamaha wako. Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka bayana ya kuwa, unaposamehe, hutakiwi kusitiri au kukana uzito wa kosa ulilofanyiwa. Msamaha haumaanishi kusahau wala haumaanishi kupuuza, au kujisingizia, makosa ambayo mtu amekufanyia au kikundi cha watu kimekufanyia. Ijapokuwa msamaha unaweza kusaidia kujenga uhusiano ulioharibika, haukulazimishi kupatana na mtu aliyekukosea au kumfanya asiwajibike kisheria kwa makosa aliyokufanyia. Badala yake, msamaha humletea yule anayesamehe amani ya moyo; na humpa uhuru kutokana na hasira aliyokuwa nayo, juu ya yule aliyemkosea.

Wataalamu wanaosoma au kufundisha msamaha huweka wazi kwamba unapomsamehe mtu, huwezi kupotezea au kukana uzito wa kosa alilokufanyia. Kusamehe ni hali fulani inayotoka ndani ya moyo wa mtu, ikiwa na hali ya uhuru wa hiari wa mtu mwenyewe kuamua kuachilia kile kinachomuumiza, pasipo kuwepo masharti ya aina yoyote ile kwa mtu aliyemuumiza.

Mungu hapendi hasira kwa sababu ni vigumu kutokutenda dhambi ukiwa na hasira.

Advertisements

From → Mengineyo

2 Comments
  1. Unaweza kushindwa kumsamehe mtu ukidhani hustahili. Lakini unastahili.

  2. Mgendi Joseph permalink

    MSAMAHA

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: