Skip to content

Bahari ya Pasifiki

31/01/2017

pasifiki

Bahari kubwa kuliko zote ulimwenguni inayotumiwa na majambazi wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusafirisha madawa ya kulevya duniani kote – Pasifiki – meli saba za Kolonia Santita zilipokamatwa zikiwa njiani kuelekea India, Marekani, Afrika Kusini na Ginebisau, Kiongozi wa Kolonia Santita Panthera Tigrisi alipokamatwa akiwa njiani kuelekea Kolombia na Gwatemala.

Meli ya kwanza kuondoka katika Bandari ya Salina Cruz kusini mwa Meksiko katika Bahari ya Pasifiki ni ‘La Diosa de los Mares’, ‘Mungu wa Bahari’, au ‘Goddess of the Seas’, Tani 6000, iliyoondoka saa tisa kamili usiku kuelekea Miami nchini Marekani; wakati ya mwisho kuondoka ilikuwa CSS (‘Colonia Santita of the Seas’, Tani 10000), na SPD (‘El Silencio Depredador del Profundo’, ‘Mnyama Mtulivu wa Kina Kirefu’, ‘The Silent Predator of the Deep’ – nyambizi ya Panthera Tigrisi), zilizoondoka saa kumi na moja alfajiri kuelekea Gwatemala na Kolombia.

Salina Cruz ni sehemu iliyopo kandokando mwa Bahari ya Pasifiki kusini kabisa mwa Meksiko, na kaskazini-mashariki kwa Reparo Jicara katika jimbo la Oaxaca. Kambi ya Panthera Tigrisi ilijengwa ndani ya Msitu wa Benson Bennett – katika ufuko wa bahari kubwa kuliko zote ulimwenguni, iliyopuliza hewa na kuyumbisha miti anuai juu ya maabara kubwa kuliko zote katika Hemisifia ya Magharibi; ya kokeini, heroini, bangi, eksitasi na hielo ya China na Kolombia. Panthera Tigrisi alikamatwa katika Bahari ya Pasifiki. Kahima Kankiriho alikamatwa katika Msitu wa Benson Bennett.

From → Picha

One Comment
  1. Kazi ya Vijana wa Tume si kuua, ni kukamata, wataua itakapobidi. Kwa hasira zake, John Murphy alitaka El Tigre (Panthera Tigrisi) auwawe na mwili wake utupwe katikati ya Bahari ya Pasifiki ili dunia imsahau milele – kwa maana ya kupoteza ushahidi wa kaburi lake. Lakini Christoffer Sortevik, Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Tume ya Dunia, aliwatuma wamkamate – ili mahakama ifanye kazi yake.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: