Skip to content

Manabii wa Uongo

27/03/2017

Manabii wa Uongo

218. Manabii wa uongo, na wafuasi wao, hawautaki ukweli. Kazi yao ni kutulazimisha tumwabudu Mpinga Kristo, badala ya Yesu Kristo, bila sisi wenyewe kujua. Wana mamlaka yote ya Mpinga Kristo kwa sababu, kama Mpinga Kristo, wanaongozwa na Shetani. Walimu hawa wa uongo wanaopenda kuvalia misurupwenye ya kisawasawa, na wanaoongea utafikiri wamemeza Biblia na kuitapika kwenye mikrofoni, lengo lao ni kutupeleka kwenye ufalme wa Shetani. Hatuna budi kuitangaza injili ya kweli ya Yesu Kristo, kwa imani ya kweli, kupata urithi usiohongeka wa ufalme wa Mungu.
 
Manabii wa uongo wana dhambi kuu tatu: tamaa ya ngono, uasi dhidi ya mamlaka ya Kristo, na dharau kwa Shetani.
 
Nabii wa uongo atampinga Shetani kwa nguvu zake zote, atakuwa na tamaa ya wanawake au wanaume kama ilivyokuwa kwa Sodoma na Gomora na miji yote iliyoizunguka miji hiyo, na atayadharau mamlaka ya Kristo.
 
Nabii wa kweli lazima awe na upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi. Kuonyesha usungura wa manabii wa injili ya woga ni jukumu la kila Mkristo wa kweli, kuokoa roho za watu wengi kwa kadiri tutakavyoweza.

 

Advertisements
One Comment
  1. Kuonyesa hila za manabii wa ghalati ni jukumu la kila Mkristo wa kweli ili kuokoa roho za watu wengi kabla Taabu ya Yakobo haijaanza.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: