Skip to content
Tags

Bunduki ya Kimarekani Iliyotumika Zaidi Katika Vita ya Vietinamu

31/03/2017

M16

Bunduki ya Kimarekani iliyotumika zaidi katika vita ya Vietinamu kati ya mwaka 1963 hadi mwaka 1969 dhidi ya Vietinamu, M16, yenye uwezo wa kubeba risasi 30 kwa wakati mmoja katika chemba yake, iliyotumiwa na magaidi wa Kolonia Santita mwaka 1992 dhidi ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya huko Mexico City nchini Meksiko.
 
Bila bunduki ya M16 John Murphy huenda angeuwawa na magaidi huko Xochimilco (‘Sochimiliko’), karibu na sanamu la karne ya kumi na sita la ‘Parroquia de San Bernardino de Siena’ jijini Mexico City, baada ya Debbie Patrocinio kumwokoa kwa kutumia mwanasesere wa nyoka wa Lisa Graciano.
 
Ndani ya chumba, akiwa bado amechanganyikiwa, akiwa hajui Debbie alikokwenda, Murphy alisikia walinzi wakipiga kelele nje. Kamanda huwa anakuwa shetani nyakati kama hizo. Alibeba pumzi. Mikononi mwake akiwa na M16, Debbie kichwani, Murphy alishangaza umati wa watu! Risasi zaidi ya thelathini zilifyatuka katika bunduki, mlango wote ukabomoka – ndani ya sekunde kumi!
 
M16 zilizotumiwa na majeshi ya Marekani dhidi ya majeshi ya Vietinamu mwanzoni hadi mwishoni mwa miaka ya sitini ziliitwa M16A1 (ya kwanza kutoka juu kwenye picha) zilizokuwa na chemba (‘magazine’) fupi zenye uwezo wa kubeba risasi ishirini kwa kila moja kwa wakati mmoja.
 
Bunduki zilizotumiwa na magaidi wa Kolonia Santita dhidi ya Vijana wa Tume zinaitwa M16A2, M16A3 na M16A4 (ya pili, ya tatu, na ya nne kwa mfuatano huo) zenye uwezo wa kubeba risasi thelathini katika chemba zake za STANAG za NATO kila moja kwa wakati mmoja.
 
Murphy, kule Xochimilco, Mexico City, alitumia bunduki mbili za M16A2 kwa wakati mmoja hivyo kutumia risasi zaidi ya thelathini ndani ya sekunde kumi.
 
Bunduki hizi, zilizoanza kufanyiwa utafiti na Chuo Kikuu cha Hopkins mara tu baada ya Vita ya Korea (1950 – 1953) kwa ufadhili wa Jeshi la Marekani, si nzuri sana kuzilinganisha na AR-15 au AK-47; lakini hakuna bunduki nzuri kuliko nyingine, zote zinafanana.
Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: