Skip to content

Bustani za Tivoli

22/08/2017

Tivoli

Bustani za Tivoli, katikati ya kituo kikubwa cha treni cha Hovedbanegård na kituo kikubwa cha mabasi cha Rådhuspladsen, ni bustani kubwa za michezo na mapumziko za Copenhagen. Bustani hizi ndizo zilizotumika kuwapoteza majambazi wa Kolonia Santita katika harakati za kumwokoa Daniel Yehuda wa bandia, katika Machafuko ya Sheraton jijini Copenhagen.
 
Majambazi wa Kolonia Santita Regner Steiner (‘Kimbunga’) na Ulla Wagner (‘Death Queen’); walivyokimbia wakiwa ndani ya magari mawili ya kihuni, Polisi wa Tume na wa Copenhagen waliwaona vizuri. Polisi waliingia katika magari yao kwa pupa na kuwafukuza maadui kwa nguvu zao zote, lakini maadui wakawashinda nguvu. Maadui walionekana kuwa mafundi stadi wa kuendesha magari, bila hata kujali watu na magari mengine mabarabarani.
 
Kimbunga alijizungusha nje ya Bustani za Tivoli kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta akiwauza kabisa polisi wa tume na polisi wa Copenhagen. Lakini Ulla, aliyekimbilia upande mwingine wa Barabara ya Søgade, hakufika mbali hata hivyo. Alizingirwa, ghafla, na magari mengine ya polisi, ambayo kwa kipindi kile yalikuwa yakitokea katika kituo kikuu cha polisi cha Tume ya Dunia kilichopo Århusgade.
Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: