Skip to content

Bahari ya Mediterania

29/08/2017

Mediterania

Bahari iliyoungana na Bahari ya Atlantiki kupitia ukanda wa bahari wa Gibraltar, iliyozingirwa kwa kiasi kikubwa na eneo la nchi kavu la Mediterania – Mediterania – Radia Hosni alipobakwa na Waturuki akiwa na umri wa miaka kumi na nne huko Bab El Jedid, Barabara ya Mohammed Ali, Sousse, Tunisia, mwaka 1976.
 
Matukio makubwa ya kusikitisha hubadilisha maisha ya watu. Akiwa na umri wa miaka kumi na nne katika mji wa Sousse, kaskazini mwa Tunisia, Radia Ja’far-Saadiq Hosni alianza mchezo wa kung’fu na kareti kwa kushurutishwa na kitendo kibaya kilichomtokea huko Bab El Jedid, Barabara ya Mohammed Ali, Januari 1976, pembezoni mwa Bahari ya Mediterania.
 
Watu watatu, watalii wa Uturuki, jioni hiyo ya tarehe 17, wakiwa wamelewa, walimteka Radia na kumpeleka mbali katika ufuko wa bahari. Walimbaka kwa zamu mpaka Radia akazimia. Kitendo hicho kilibadilisha maisha ya Radia kabisa. Kilimsumbua kwa muda mrefu. Alipopona Radia ndipo alipokata shauri na kujiunga na chuo cha karibu na nyumbani kwao cha kung’fu na kareti cha Place des Martyrs, karibu na jumba la halmashauri ya mji, ili akionana tena na Waturuki asionewe tena.
 
Miaka minne baadaye, akiwa na umri wa miaka ishirini, Radia alihamia Tunis kwa shangazi yake akiwa na mikanda miwili myeusi: wa kung’fu, ya China, na kareti ya Japani. Alipomaliza chuo kikuu, Radia alijiunga na Kitengo cha Usalama wa Taifa cha Majeshi ya Ufaransa (CERM) kwa muda (‘secondment’) kutoka Usalama wa Taifa wa Tunisia.
 
Akiwa CERM, ‘Centre d’Exploitation du Renseignement Militaire’, Radia alifanya kazi kwa bidii na utiifu mkubwa kiasi cha sifa zake kumfikia mnadhimu mkuu wa majeshi ya Ufaransa (CEMA), aliyempendekeza kwa majemadari wa Kikosi cha Anga cha Kikomandoo cha Uingereza (SAS – ‘Special Air Services’) ili wamchukue (kwa mazungumza na Serikali ya Tunisia) kipindi uhamisho wake utakapokwisha Strasbourg nchini Ufaransa.
 
Alipomaliza mafunzo yake ya ukomandoo Hereford nchini Uingereza, Radia alirudi Tunisia na kulitumikia jeshi la nchi yake (TAF – ‘Tunisian Armed Forces’) kwa miaka miwili kabla ‘dunia’ haijamuomba kujiunga na Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya kama mpelelezi-mwanajeshi-komandoo wa Executive Action Corps, mwaka 1987.
 
Kutokana na mkataba wa kisheria wa kimataifa wa WODEC (‘WODEA Statute’), WODEC ilimpa Radia dola za Kimarekani milioni moja kumfanya awe mfanyabiashara – kama motisha na kuficha utambulisho wa kazi yake halisi kwa sababu za kiusalama.
 
Akijulikana kama mfanyabiashara wa maduka ya nguo na vipodozi jijini Tunis, na kachero wa Tume ya Dunia jijini Oslo; Radia Hosni, 31, ni miongoni mwa mashujaa adimu waliowahi kukanyaga ardhi ya Tunisia.
Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: