Skip to content

Kusafisha Kuanzia Ndani Kuja Nje Ndilo Jibu la Matatizo ya Nje

25/09/2017

Madaktari

244. Madaktari wa duniani hutibu matokeo ya ugonjwa. Lakini Yesu hutibu chanzo. Hivyo Yesu ndilo jibu la matatizo ya duniani. Anasafisha kuanzia ndani kuja nje. Kusafisha kuanzia ndani kuja nje ndilo jibu la matatizo ya nje.

Tunapojifunza na kulipokea Neno la Mungu tunakuwa karibu na yule anayeweza kutupa maarifa na nguvu ya kupambana na adui yeyote wa kiroho. Maana Neno la Mumgu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo (Waebrania 4:12).

Yesu Kristo huponya kwa kutumia tiba ya Neno la Mungu na tiba hiyo ni ya milele! Hutaweza kwenda mbinguni bila viza, hutaweza kuponya au kupona bila Neno la Mungu, na hakuna Mungu bila Yesu. Yesu, kaka yetu mkubwa, ni viza ya kwenda mbinguni.

Advertisements
Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: