Skip to content

CS-Copenhagen

28/10/2017

Copenhagen

Copenhagen; jiji kubwa kuliko yote katika nchi za Skandinavia na mji mkuu wa Denmaki; Makao Makuu ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya – WODEC; na makao makuu ya tawi kubwa kuliko yote ya Kolonia Santita duniani, CS-Copenhagen.
 
CS-Copenhagen ilikuwa na mamlaka katika nchi za Baltiki kama vile Estonia, Lativia na Litwania; Skandinavia kama vile Denmaki, Swideni, Norwe na Aisilandi; Ulaya ya Kaskazini kama vile Denmaki, Estonia, Ufini, Aisilandi, Ayalandi, Lativia, Litwania, Norwe, Swideni na Uingereza; na baadhi ya nchi za Ulaya ya Kati kama vile Uswisi, Ujerumani, Hungaria na Polandi.
 
CS-Copenhagen ilikuwa na viongozi wafuatao: Regner Steiner Valkendorff “The Storm” au “Kimbunga” (kwa sababu alipeperusha watu); Ida Taico “Weasel Girl” Nidhug; Marcus Overgaard “The Don”; Karen Karlsen; Ulla Wagner “Death Queen”; Banke Mohamed, na Peter Honore mwenye asili ya Ufaransa.
 
Valkendorff aliiendesha CS-Copenhagen kwa muda wa miaka mitatu na nusu, kabla ya kuuwawa kwa MP5 ya John Murphy huko Meksiko mwaka 1992. Regner, ambaye jina lake humaanisha “shujaa mwenye hekima”, alikuwa na umri wa miaka 38. Alizaliwa mwaka 1954, Machi 16. Hadi kifo kinamkuta, alikuwa na rafiki wa kike na watoto wawili kwa mke wake wa zamani.
 
Baada ya kifo cha Valkendorff huko San Antonio, Mexico City, CS-Copenhagen ilisambaratishwa rasmi na WPD. WPD (“WODEC Police Department”) ni Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya, yenye mamlaka ya kikatiba katika nchi 143 za WODEA. WODEA (“World Drugs Enforcement Administration”) ni Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya na Ugaidi wa Kimataifa Duniani.
Advertisements

From → Picha

Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: