Skip to content
Tags

Chuki ya Mwanamke

06/11/2017

Mwanamke

250. Kuna vitu vitatu katika maisha ambavyo havina kiasi katika kutenda mema au mabaya: kanisa, mwanamke, na ulimi. Kanisa na ulimi vina uwezo wa kujenga, na vina uwezo wa kubomoa kulingana na jinsi vitakavyotumika. Mwanamke anapozidisha ubaya anakuwa mbaya kwelikweli, na anapozidisha wema anakuwa mwema kwelikweli. Kwa kuwa ubavu uliomuumba mwanamke umejipinda, usilazimishe kuunyoosha.
 
Mwanamke ama apende au achukie; na akipenda anapenda kwelikweli, akichukia anachukia kwelikweli. Na machozi ya mwanamke ni machozi ya kilaghai; kwani yanaweza kutokana na huzuni ya kweli, au yanaweza kutokana na huzuni ya kilaghai. Mwanamke anapopata muda wa kufikiria, aghlabu hufikiria maovu.
 
Chuki ikizidi inazaa uchawi na hakuna uchawi mbaya kama uchawi wa mwanamke. Mwanamke ni mchawi kwa sababu ana udhaifu zaidi kiimani kuliko mwanamume, na kwa sababu lengo kuu la Shetani ni kupotosha imani, kwa hiyo Shetani anaona ni vema amshambulie mwanamke ambaye ni dhaifu kuliko kumshambulia mwanamume. Mwanamke ni mwepesi zaidi kuathiriwa na nguvu za giza kuliko mwanamume, na anapozitumia nguvu hizo vibaya anakuwa mbaya kwelikweli.
 
Lakini sababu kubwa ya mwanamke kuwa na chuki ni Hawa. Hawa ndiye binadamu wa kwanza kabisa kutenda dhambi duniani, ijapokuwa dhambi yake ilifutwa kwa baraka ya Maria Magdalena mama yake na Yesu. Dhambi ya Hawa ni dhambi ya asili. Kama ilivyo wazi kutokana na machukizo mengi ya kimwili ya mwanamke, mwanamke ana tamaa zaidi za kimwili kuliko mwanamume.
 
Hapo mwanzo wakati Mungu anaumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo, kulikuwa na “kasoro” katika uumbaji wa mwanamke wa kwanza; kwani Hawa aliumbwa kutokana na ubavu uliojipinda wa Adamu. Kupitia kasoro hiyo mwanamke ni binadamu asiyekuwa na ukamilifu, ni binadamu hodari sana wa udanganyifu. Anapolia, mwanamke huwa anatega mtego. Huwa anakuwa na njama za kumdanganya mwanamume, kama Delila alivyomdanganya Samsoni.
 
Delila alimshawishi Samsoni amwambie kitendawili alichowapa Wafilisti, na akawapa jibu. Hivyo, Delila akawa amemdanganya mumewe.
 
Na ni wazi katika kesi ya mwanamke wa kwanza kwamba, Hawa alikuwa na imani kidogo. Kwani nyoka alipouliza kwa nini hawakula matunda ya kila mti bustanini alimwamini nyoka badala ya kumwamini Mungu, aliyesema wasile baadhi ya matunda bustanini.
 
Lakini yote haya yanaonyeshwa na elimu ya asili na historia ya neno la Kilatini liitwalo “femina”. “Femina” (“female”) hutokana na neno “fe” (ambalo humaanisha “fides” au “faith” au “imani”), na neno “minus” (ambalo humaanisha “less” au “dogo zaidi”). Kwa hiyo, “mwanamke” maana yake ni “imani ndogo”. Ndiyo maana mwanamke ni dhaifu kudumu na kushika imani, na ndiyo maana Shetani anamwonea sana.
 
Hata hivyo, dunia ni mwanamke. Bila mwanamke sisi wote tusingekuwepo. Mwanamke aliumbwa kutokana na ubavu wa mwanamume, si kutokana na miguu ya mwanamume ili mwanamume amkanyage, wala si kutokana na kichwa cha mwanamume ili mwanamume awe juu yake. Aliumbwa kutokana na ubavu wa mwanamume ili awe msaidizi wa mwanamume, chini ya mkono wa mwanamume ili mwanamume amlinde, na kando ya moyo wa mwanamume ili mwanamume ampende.
 
Kuwa mkarimu kwa mwanamke, kwani aliumbwa kutokana na ubavu uliojipinda; na sehemu iliyojipinda zaidi ya ubavu huo ni ya juu, inayofanya iendelee kujipinda daima. Maana yake ni kwamba atakuwa na chuki maisha yake yote.
 
Kwa kuwa ubavu uliomuumba mwanamke umejipinda, ukilazimisha kuunyoosha utauvunja.
Advertisements
Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: