Skip to content
Tags

Huwezi Kumlazimisha Mungu Afanye Kitu Unachotaka Afanye

13/11/2017

Mungu

251. Huwezi kumlazimisha Mungu afanye kitu unachotaka afanye. Mathalani, unaweza kumpeleka mgonjwa kwa mchungaji akaombewe. Mgonjwa atapona Mungu atakapoamua apone.

Shetani ukimwomba kitu, kama umesaini naye mkataba, anakupa hapohapo. Mungu ukimwomba kitu anaweza asikupe, kwani akikupa utakuwa muujiza ambao Mungu anaufanya kwa muda anaotaka yeye, na si muda anaotaka mwanadamu. Kwa hiyo huwezi kusema kwamba Mungu anaondoa uchawi wakati hujui kama ataondoa au hataondoa.

Bikira Maria alipomwomba Yesu afanye muujiza wa divai katika harusi huko Kana, Galilaya, Yesu alimshangaa na akasema saa yake ya kufanya muujiza ilikuwa bado haijawadia (Yohana 2:4). Mama na Mwana walikuwa na ushirika gani kati yao katika kutenda muujiza wa divai? Mama alitaka muujiza ufanyike hapohapo, lakini Mwana alikuwa na muda wake wa kuufanya muujiza huo.

Aidha, inaonekana kwamba ni mara chache sana kwamba wanaume hutolewa mapepo kwa kuomba msaada wa Mungu au sala za Watakatifu. Kwa hiyo inaonekana kwamba wanaweza tu kutolewa mapepo kwa msaada wa mapepo mengine, na ni kinyume cha sheria kutafuta msaada huo.

Mungu hakupi unachotaka. Anakupa unachostahili kupata. Wachungaji wangekuwa na uwezo wa kuondoa mapepo hapohapo, kila mgonjwa angekuwa anapona hapohapo.

Tatizo, hata hivyo, ni kwamba watu wengi hawajui kuomba! Ukiomba kitu ukapata kama ulivyoomba, kwa muda uliotaka, umepata kitu ambacho Roho wa Mungu alikuongoza kuomba. Kwa hiyo, usiache kumwambia Mungu akufundishe kuomba.

Wachungaji wanapaswa kuondoa mapepo kwa kidole cha Mungu na si kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo.

 

Advertisements
Leave a Comment

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: