Skip to content

WODEA

WODEA (World Drugs Enforcement Administration) ni shirika la kujitegemea la kimataifa – linalofanya kazi kwa niaba ya Umoja wa Mataifa – lenye nia/shabaha ya kukomesha (katika dunia) madawa haramu ya kulevya, ya madaraja yote, pamoja na ugaidi wa kimataifa wa aina zote – hasa wa kimadawa, kisiasa na kinyukilia; kwa ajili ya amani, afya na usalama wa kimataifa. WODEA ilianzishwa chini ya Mkataba wa Kisheria wa Kimataifa wa WODEA (WODEA Statute) uliosimamiwa kwa kipindi cha siku tatu mfululizo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UNSC, Novemba 1975. Tofauti na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Nyukilia, IAEA, ambalo huwajibika kwa UNSC na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa; WODEA huwajibika kwa UNSC na Baraza la Uchumi na Ustawi wa Jamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC.

WODEC, Chombo Kikuu cha WODEA, ambayo hutumika kama kongamano la majadiliano ya masuala ya madawa na ugaidi ya kimataifa; huundwa na vyombo vingine vidogo vitatu: Bodi ya Makamishna ya Tume ya Dunia (WBC – WODEC Board of Commissioners), Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia (WGC – WODEC General Conference) na Sekretarieti ya Tume ya Dunia. WBC ni Chombo cha Sera cha Tume ya Dunia. Kina wajumbe 12 wanaoteuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na 26 wanaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa Tume ya Dunia. Wajumbe 12 (watano wa kudumu wa UNSC na saba viongozi wa kanda za WODEA) huteuliwa na UNSC kwa kipindi cha miaka mitano wakati 26 huchaguliwa na WGC kwa kipindi kimoja cha miaka miwili. WBC hutoa mapendekezo kwa WGC kuhusu bajeti na shughuli zote za WODEA.

Rais wa WODEA huchaguliwa na WGC kwa mapendekezo ya UNSC. WBC hupendekeza majina sita kwa UNSC ambayo huchagua majina matatu kati ya hayo sita na kuyapeleka katika Mkutano Mkuu wa WODEA – kupigiwa kura ya Kamishna Mkuu wa WODEC na Rais wa WODEA kwa kipindi cha miaka mitano. Kamishna Mkuu wa WODEC ni Rais wa WODEA. Wakati WBC hukutana mara nne kwa mwaka mjini Copenhagen kuanzia Novemba, WGC (nchi wanachama 143) hukutana mara moja kwa mwaka katika mwezi wa Novemba kuidhinisha bajeti na mapendekezo ya WBC – kwa ajili ya Sekretarieti ya Tume ya Dunia.

Sekretarieti ya Tume ya Dunia huwajibika na utekelezaji wa mapendekezo yote yaliyopitishwa na WBC na WGC kwa niaba ya WODEA. Huchaguliwa na WBC na kuidhinishwa na WGC kwa kipindi cha marudio cha miaka mitano. Sekretarieti ya Tume ya Dunia huwajibika pia na nguvukazi ya watu zaidi ya 7,000 duniani kote na bajeti ya wastani wa dola za Kimarekani milioni 400 kwa kwaka mzima.

Mbali na WBC, WGC na Sekretarieti ya Tume ya Dunia, WODEC ina vyombo vikubwa vitatu vya dola: Idara ya Polisi ya Tume ya Dunia (WPD), Idara ya Usalama ya Tume ya Dunia (WIS) na Kikosi Maalumu cha Kikomandoo cha Tume ya Dunia (EAC). EAC iliundwa kwa makubaliano maalumu ya Azimio la Copenhagen kati ya WODEA na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa – Novemba 1980.

WODEC ina maabara tatu za kikemia, ofisi tatu za mahusiano mema (Vienna, Pretoria na New York), kliniki saba za madawa ya kulevya na kanda sita katika mabara sita ya dunia nzima. Kila kanda ina bodi ya wakurugenzi, idara ya polisi, usalama, sekretarieti, maabara na kliniki za madawa ya kulevya. Kanda ya Afrika ya Kusini ya Tume ya Dunia huanzia Somalia mpaka Kameruni mpaka Afrika Kusini. Kanda ya Afrika ya Kaskazini ya Tume ya Dunia huanzia Eritirea mpaka Nijeria mpaka Tunisia, isipokuwa Moroko ambayo iko katika kanda ya Ulaya.

Advertisements
242 Comments
 1. Wonderful article! That is the type of info that should be shared around the net.
  Shame on the search engines for not positioning this put up upper!
  Come on over and consult with my website . Thank you =)

 2. It’s going to be ending of mine day, except before ending I am reading tthis fantastioc pjece of writing to increase my know-how.

 3. Hello just wanted to give you a quick heads up andd
  let you know a few of the pictures aren’t loading correctly.
  I’m not sure why but I think its a linking issue. I’ve tried it in ttwo different browsers aand both show the same outcome.

 4. It’s remarkable to pay a visit this site and reading the views
  of all mates about this paragraph, while I am also eager of getting familiarity.

 5. continuously i used to read smaller posts which as well clear their motive, and that
  is also happening with this article which I am reading
  here.

 6. ТҺis piece of writing ѡill help tthe internet visitors fߋr
  building uρ new webpage or even ɑ weblog from start tߋo end.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: